Bismillah Al-Rehman Al-Raheem
AlFatwa International 28 (Swahili)
Mwisho wa utume
Uongo mwingine wa Qadiani wafichuka!
Na Dr. Sayyid Rashid Ali
Utangulizi
Ndugu wasomaji
Assalam alaykum
Waislamu, tangu wakati wa Mtume Muhammad(s.a.w) hadi hii leo wanaamini pasi na tone la shaka kuwa hitimisho la utume ni Muhammad(s.a.w), na kuwa Qur'an ndio mwisho wa ujumbe wa Allah ulioletwa kuwaongoza Wanaadamu mpaka siku ya Kiyama.
Dhana ya mwisho wa ujumbe na utume ni tofali muhimu sana katika jengo zima la Uislamu, inayobeba nafasi muhimu sana katika maisha binafsi ya Muislamu na yale ya jamii kwa ujumla, inayojenga mahusiano ya kidugu yanayovuka mipaka ya kijiografia, rangi na mila. Udugu huu wa kiulimwengu unaojengwa na Uislamu unaufanya umma wote kuwa mmoja kama mwili mmoja, kiasi kwamba sehemu yoyote ya mwili huo inapopatwa na maumivu basi mwili mzima hutaabika.
Hiki ndicho kikwazo na pigo kubwa kwa maadui wa Uislamu ambao wamekuwa wakijaribu kila wawezavyo kuharibu jengo hilo la umoja na udugu tangu wakati wa Mtume(s.a.w) hadi hivi leo. Maadui wa Uislamu katika zama hizi, wamekuwa wakijaribu kuwagawa Waislamu kwa kutumia mbinu kuu ya kupotosha mafundisho ya Qur'an na kuchapisha maandiko yanayochafua shakhsia ya Mtume(s.a.w).
Akizungumzia hilo, Mwandishi Al Hafidh Bashir Masri katika makala yake anasema:
"Popote maadui wa Uislamu walipopanga kushambulia mizizi ya Uislamu, walijaribu kuhoji uthabiti wa Qur'an na kuchafua shakhsia ya Mtume (s.a.w). Tunapigwa vita hivyo kutoka nje. Tatizo hasa linalojitokeza hata hivyo ni pale miongoni mwetu wanapoasi kama walivyofanya Makadiani. Waweza kujikinga na hatari unayoiona, lakini ni rahisi kugongwa na nyoka aliyefichama kwenye nyasi. Na hivi ndivyo inavyojitokeza kwa baadhi ya Waislamu"
Imani ya Waislamu
Imani ya Waislamu juu ya Mwisho utume imewekwa wazi katika Qur'an. Hapa tunanukuu aya moja inayobainisha hilo.
Hakuwa Muhammad baba wa yeyote kati ya wanaume wenu. Lakini yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mwisho wa Mitume. Na mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu(33:40).
Kanuni ya msingi katika kutafsiri aya za Qur'an ni kutafsiri kwa kutumia aya kwa aya au kutafsiri kwa kutumia mafundisho ya Mtume(s.a.w) na mwisho kutumia kauli za masahaba wake.
Katika aya tuliyoinukuu hapo juu neno Khatam limefasiriwa kama Mwisho. Kilugha neno hili maana yake ni Muhuri au Rakili, kitu kilicho kilichopigwa muhuri na kufungwa barabara. Katika Qur'an zipo aya nyingi zinazothibitisha tafsiri hii ya Neno Khatama na kwa hivyo mwisho wa utume na ujumbe wa Allah kwa Wanaadamu.
Khutba ya Mwisho
Katika Khutba ya Miwisho aliyoitoa kwenye uwanja wa Arafa wakati wa Hija yake ya mwisho, Mtume(s.a.w) alisema.
"Enyi watu! Hapana Mtume atakayeinuliwa baada yangu na hapatakuwa na umma mpya baada ya huu wenu(Taz. Seerat Ibn Hisham, khutba ya mwisho).
Katika vitabu vya Hadithi
Vitabu mbali mbali vimenukuu Hadithi za Mtume(s.a.w) zinazosisitiza kuwa yeye ndiye Mwisho wa Utume. Hapa tungependa kunukuu Hadithi Sahihi iliyotumia neno Khatam:
"Kutatokea wadanganyifu thalathini katika uma wangu, kila mmoja miongoni mwao atadai kuwa yeye ni Mtume, lakini jueni kuwa MIMI ndiye Khatama Nabiyyiin, hapatakuwa na Mtume baada yangu.(Sunan Abu Daud, Kitab al Fitan).
Mtume(s.a.w) katika Hadithi hii ametumia neno Khatam un Nabiyyin kwa kujinasibu nalo yeye Mwenyewe na akatilia mkazo kwa kuongeza kuwa "Hapana Mtume baada yangu". Ni wazi Mtume alijua kuwa kutatokea wenye akili twevu katika watu wa umma wake watakaojaribu kutafsiri vibaya neno hilo.
Udanganyifu Nambari 1 wa Kadian- Madai ya Utume
Baada ya kueleza imani ya Waislamu juu Mwisho wa Utume, sasa hebu tuone imani ya makadiani juu ya Khataman un Nabiyyin, mwisho wa Utume?
Unapozungumza na Kadiani yeyote yule atadai kuwa yeye naye anaamini kuwa Mtume Muhammad ndiye mwisho wa Mitume. Hata hivyo unafiki wake hufichuka pale tu utakapomuuliza anamaanisha nini anapotamka neno Khaataman Nabiyyin. Baada ya hapo udanganyifu wake hudhihirika kwa sababu ana ueleo wake binafsi wa neno hili kama alivyofundishwa na jumuiya yake. Kwa kila Kadian, Khatama un Nabiyyin ina maana zifuatazo:
. Ni Muhuri wa Manabii lakini si Muhuri umaanishao mwisho wa Utume(kama waaminivyo Waislamu) ila ni idhinisho la utume
. Mmbora wa Mitume.
Katika kuthibitisha dai lao hutoa maelezo marefu kushikilia msimamo wa kijinga usio na mantiki. Suala hili linatukumbusha jinsi kazi ya Mirza ilivyo na undumakuwili; sehemu ikidai kuunga mkono mafundisho ya jumla ya Uislamu ikionesha pia maana ya Khatam kuwa ni mwisho na sehemu nyengine ikikana na kubadilisha maana ya Muhuri wa Mitume kuwa ni idhinisho la utume. Mirza kwa dhahiri yake ametumbukiza dhana za kishetani katika mfundisho yake aliyodai kuwa ni Uislamu. Katika sehemu kadhaa za mafundisho yake amedai kuwa hapana Mtume baada ya Muhammad, alifanya hivyo kama janja ya kuunganisha mafundisho yake na Uislamu ili kuyafanya yakubalike. Hata hivyo sehemu nyingine ametoa maelezo ya wazi kabisa akipinga mwisho wa Utume na kudai kuwa kutakuwa na Mitume watakaokuja baada ya Muhammad.
Mirza ametumia janja hii ili kwa sura ya nje ionekane kuwa Ahmadiya wanaamini sawa na Waislamu wengine lakini kwa ndani apotoshe mafundisho haya kwa kutumbukiza dhana zake za kishetani. Makadian wanadai kuwa Mirza hakutaja kuwa yeye ni Mtume, wanatoa nukuu za maandiko kuthibitisha hilo. Pia wandai kuwa alijitaja yeye ni Mtume kadhalika wanatoa nukuu kadhaa kuthibitisha hilo. Wametumia njia hii hii sura mbiliza ukweli ili kuwazuga watu. Kwa hiyo wanweza kuttoa malezo kudai kuwa Khatam maana yake ni Mwisho lakini wakati huo huo wanaweza kutoa maelezo yanayothibitisha na rejea zao kadhaa kuwa Khatam maana yake ni idhinisho la Utume kwa kutakuwepo na mitume wengi watakaokuja.
Nukuu zinazoonesha kukana kwa Mirza kuwa yeye si Mtume
"Je anaweza akawepo mzushi atakayedai kuwa yeye ni Mtume na mjumbe wa Mwenyezi Mungu akiiamini Qur'an, na mtu huyo akadai kuamini Qur'an na aya isemayo "Walakin Rasuulallah Wakhaataman Nabiyyin" kuwa ni neno la Mwenyezi Mungu, bado akaamini vile vile kuwa mimi nami ni Mtume na mjumbe wa Allah baada ya Mtume mtukufu(s.a.w)?(Anjam Atham, Roohani Khazain Juzuu 11 uk. 27)
"Nafahamu kwamba chochote kinachopingana na Qur'an ni cha uongo, rida(kuritadi) na kisicho na ithibati, hivyo ni kwa vipi mimi nidai utume hali ya kuwa ni Muislamu?"(Hamamatul Bushra, Roohan Khazain juzuu ya 7 uk. 297).
"Enyi watu msiwe maadui wa Qur'an na baada ya Khaataman Nabiyyin msianzishe mfumo mpya wa ufunuo wa kitume. Mumuonee haya Allah kwa yeyote yule atakayekutokezeeni".(Asmani Faisla, Roohan Khazain juzuu ya 4 uk. 335).
Licha ya maelezo hayo, Mirza kwa upande mwingine alifuma mantiki ya upotoshaji kuhalalisha madai yake ya Utume.
"Mwenyezi Mungu alihisi kwamba katika zama hizi kutafika wakati atakaohitajika Mujadid mkubwa kwa hiyo muhuri(idhinisho) la Mungu litafanya kazi ya kuwaidhinisha wafuasi wa Mtume wafikie daraja itakayowafanya wakati fulani waonekane ni umati wake na wakati mwingine waonekane ni Mitume, kwa sababu Mwenyezi Mungu amemfanya Mtume(s.a.w) kuwa shahidi wa Muhuri ya kwamba amempiga chapa ya Muhuri ili kumfanya awe mkamilifu zaidi..."(Haqiqatul Wahi, Roohan Khazain juzuu ya 22 uk. 99-100).
"Maana ya Khataman Nabiyyin ni hii kwamba bila muhuri wake hapana utume wa yeyote unaoweza kuthibitishwa. Ni kwa kugongwa Muhuri tu ndipo usahihi na uthabiti wa karatasi unapoonekana."(Malfoozat e- Ahmadiyya juzuu ya 5 uk. 290).
Kimahubiri, kwa maneno mengine Khaataman Nabiyyin kwa Mtume(s.a.w) inaashiria daraja kubwa na ni kwa maana hii yeye amekuwa Muhuri wa Mitume, ikiwa na maana kwamba baada yake watazaliwa mitume ambao sharti lao ni kumfuata yeye."(Barua ya Mian Mahamood, Khalifa wa Qadian, AlFazl Qadian ya tarehe 29 Aprili 1927).
Kwa hakika mpinzani wetu Moulvi Sahebaan amefanya makosa makubwa katika kuelewa maana ya Khatamn Nabiyyin, Yeye(Muhammad (s.a.w) ni Khataman Nabiyyin kwa maana kwamba amefanywa kuwa Muhuri wa idhinisho kwa Mitume."(ALFazl Qadian tarehe 8 Desemba 1915).
"Hatupingi kwamba Mtume(s.a.w) ni Khaataman Nabiyyin lakini maana ya Khatam si ile wanayoilewa Waislmu wengi ambayo inapinga utukufu wa Mtume Muhammad(s.a.w) kwamba ameunyima fursa umma wake ya utukufu wa Utume.(AlFazl Qadian tarehe 22 August 1939).
"Hapana yeyote katika Ulimwengu anayeweza ukweli halisi wa Khaataman Nubuwway wa Muhammad ila yule ambaye ni Khatam ul Awliya kama Hazrat Khataman Anbiyya, kwa sababu kuelewa ukweli halisi wa kitu kunategemea kustahiki kwa mtu katika kitu hicho na ni ukweli uliothibitika ni kwamba mtu anayestahiki Khatimiya ni ama Mtume(s.a.w) au Hazrat Masihi Mowood(Mirza Saheb."( Taz.Jarida la Qadian Tasheed ul Azhan, Na. 8, juzuu ya 12, uk.201 chini ya mada iliyopewa kichwa "Ukweli halisi wa Khatmi Nubuwat wa Muhammad, la mwezi Agosti 1917).
Udanganyifu nambari 2 wa Kadian- Maana ya Khatam:
Makadiani wamekuwa wakitoa vijisababu vingi kuhalalisha maana yao ya neno Khatam. Wanadai neno Khatama limetumika kama ifuatavyo:
1. Khaatama ush-Shu'Araa(Muhuri wa Washairi) ambayo imetumika kwa mshairi Abu Tammam. (Taz. Wafiyatul A'yan, juzuu. 1, uk. 123, Cairo).
2. Khataman ush Shuaraa vile vile limetumika kwa Abul Tayyeb. (Muqaddama Deewanul Mutanabbi Misri uk. 4).
3. Khataman ush Shuaraa vile vile limetumika kwa Abul A'la Alme'ry(tazama rejea hiyo hiyo, uk.4 katika footnote(tanbihi)
4. Khataman ush Shuaraa limetumika kwa Sheikh Ali Huzain wa India. Hayati Sa'd, uk.117)
5. Khataman ush Shuaraa limetumika kwa Habeeb Shiraza wa Iran. (Hayat Sa'd, uk. 87) cha kuzingatia hapa ni kwamba watu wote watano wamepewa hadhi hiyo. Ni namna gani neno hilo laweza kutafsiriwa kuwa "mwisho". Hawa hawakujitokeza wala kwenda wakati mmoja.
6. Khatam ul Auliya-(Muhuri wa watakatifu) limetumika kwa Hazrat Ali(r.a). (Taz. Tafsir Safi, sura ya AlAhzab) je yupo hivi leo yeyote yule anayeweza kufikia Wilaayat iwapo maana ya Khatam ni mwisho?
7. Khatama Al Auliyaa- limetumika kwa Imamu Shafii. (Taz. Tuhfatus Sunniyya, uk. 45).
8. Khataman Auliyaa- limetumika kwa Sheikh Ibnul 'Aarbee.(Fotohat Makiyya).
9. Khatam Al Karaam
10. Khataman Al Ilmu Al Aimmah(Muhuri wa viongozi wa dini) limetumika kwa Imam Muhammad Abdah wa Misri.(Tafseer Alfatehah, uk.148) je leo hatuna viongozi?
11. Khatam Atul Mujahediin(Muhuri wa Mujahidiin) limetumika kwa AlSayyad Ahmad Sanosi. Akhbar AlJamiatul Islamiyya, Palestina, 27 Muharram, 1352)
12. Khatama Al Muhaqqiqiin(Muhuri wa wasomi watafiti) limetumika kwa Ahmad Bin Idrees. (Al'Aqadum Nafees)
13. Khatam tul Ulamaa Al Muhaqqdiqiin(Muhuri wa Watafiti0 limetumika kwa Abul Fazl Aloosi.
14. Khatama Al Muhaqqiqiin limetumika kwa Shaikh Al Azhar Saleem Al Bashree. (Al Haraab, uk. 372)
15. Khaatam tul Muhaqqiqiin limetumika kwa Sheikh Imam Suyuut.
16. Khaataman al Muhaddithiin(muhuri wa wapokezi) limetumika Shah Waliyyullah wa India.
17. Khamatamal Huffaz (muhuri wa Mahaafidh). Limetumika kwa Sheikh Shamsuddin
18. Khataman Al Aulia(muhuri wa Watakatifu) limetumika kwa Mtakatifu wa juu. (Tazkiratul Auliyaa, p Ghaib422.
19. Khatama Al Aulia limetumika kwa Watakatifu waliopiga hatua za mafanikio. (Fatoohul Ghaib, p43)
20. Khatama Atul Fuqaaha(Muhuri wa Majaji) limetumika kwa Al Sheikh Najeet.(Akbaar Siraat al Mustaqeem Yaafaa, 27 Rajab, 1354 A.H).
21. Khatama al Mufassireen (Muhuri wa wa Wafasiri) limetumika kwa Shaikh Rasheed Raza. (Al Jaameemiatul Islamia, 9 Jamadiy Thaan, 1354 A.H)
22. Khatama atul Fuqaha limetumika kwa Shaikh Abdul Haque.(Tafsirul Akleel)
23. Khatama Al. Muhaqqeen(Muhuri wa Watafiti limetumika kwa Ashaikh Muhammad Najeet, (Al Islam Asr Shi'baan 1354 A.H).
24. Khataman Al Wilaaya(Muhuri wa utakatifu) kwa mbora wa Watukufu).(Muqaddima ibni Khuldoon, p 271).
25. Khatama Al Muhaddithiin wal Mufassiriin(Muhuri wa wapokezi na Wafasiri) limetumika kwa Shah 'Abbdul' Azeez.(Hadiyyatul Shi'ah)
26. Khatamn Al Makhlooqaat Al- Jismaaniyyah(Muhuri wa maumbile) limetumika kwa Wanaadamu. (Tafsiir Kabeer, juzuu 2, p.22, imechapishwa Misri)
27. Khatam-Atul-Huffaz limetumika Shaikh Muhammad Abdullah.(AlRisaail Naadirah, uk.30)
28. Khatam Atul Muhaqqiqiin limetumika kwa Allama Sa'adudiin Taftazaan. (Shra Hadiithul Arbaiin, uk1)
29. Thatama Atul Hufaaz limetumika kwa Ibn Hajrul Asqalaan.(Tabqatul Madlaseen).
30. Khatam Al Mufassiriin(Muhuri wa Wafasiri) limetumika kwa Maulana Muhammad Qaassim.(Israare Quraan).
31. Khataman Al Muhaddithiin(Muhuri wa Wapokezi)limetumika kwa Imamu Suyuut. (Hadiyatul She'eah, uk. 210)
32. Khatama Al Hukkaam(Muhuri wa Watawala) limetmika kwa Wafalme).(Hujjatul Islam, uk.35)
33. Khataman Al Kaamiliin(Muhuri wa wakamilifu) limetumika kwa Mtume(Hujjatul Islam, uk. 35).
34. Khataman Al Miraatab(Muhuri wa vinyago) kwa vinyango vyene taswira ya watu). Ilmu Kitaab, uk. 140).
35. Khatam Al Kamaala(Muhuri wa miujiza) limetumika kwa Mtume(s.a.w)(ibid 140)
36.Khatam al Asfiyaat al Immah(Muhuri wa maruhani wa Taifa) limetumika kwa Issa (A.S). (Baqiyyatul Mutaqaddimiin), uk 184).
37. Khatama Al Ausiyaa(Muhuri wa watoa Nasaha, Washauri) limetumika Sahaba Ali)(Minar Hudaa)
38. Khatam Al Mua'llimiin(Muhuri wa Waalimu/ Wasomi) limetumika kwa Mtume(s.a.w). (Alsiraatul Sawee na Allama Muhammad Sabtain,sasa, mimi ni mwalimu, na mnajua kwamba nitabaki kuwa hivyo, baada ya Mtume(s.a.w) lakini wakati wote ninakaribi kuwa mwalimu kwa ukamilifu zaidi kama alivyokuwa alivyofanya. Ni namna gani angeweza kuwa Muhuri wa mwisho wa Waalimu maana yake yeye ni mbora si wa mwisho.
39. Khaatamn Al Muhaddithiin(Muhuri wa Wapokezi) limetumika kwa Al Shaikhul Sadooq.(Kitaab Man Laa yahdarahul Faqiih).
40. Khatam Al Muhaddithiin, limetumika kwa Maulana Anwar Sjha wa kashmir.(Kitab Raeesul Ahrar)
Katika mifano yote hiyo iliyotolewa na Mirza hakuna hata rejea moja ya Hadithi za Mtume(s.a.w) iliyotumika kuthibitisha madai hayo. Kwa nini?
Kwa nini Makadiani wameziondoa Hadithi hizi?
Ingawa kila Kadiani akiwemo Mirza mwenyewe, wanadai kwamba wanaamini Qur'an na Hadithi na wanampenda Mtume(s.a.w), bado wamezipuuza hadithi hizo, ambazo zinzkanusha kwa uwazi kabisa madai ya Mirza Ghulam Ahmad, Qadiani. Uthibitisho uko katika nukuu ifuatayo inayotokana na kitabu cha Mirza:
"Msingi wa madai yetu sio Hadithi za Mtume wala Qur'an bali ni Wahyi ulionijia. ndiyo, katika kuunga mkono vile vile tunawasilisha Hadithi hizo ambazo ni kwa mujibu wa Qur'an na hazigongani na Wahyi wangu, hadithi zilizobaki nazitupilia mbali mitihili ya karatasi chafu"(Roohan Khazain Vol. 19 uk. 140).
Nukuu hiyo inaonesha sura halisi ya Mirza Qadian na harakati zake za Ahmadiyya. Hadithi yoyote inayopingana na madai ya Mirza hutupiliwa mbali mithili ya takataka. Mtu mwenye dharau kama hii bado anadai kumpenda na kumfuata Mtume Muhammad(s.a.w).
Kitu kingine!, rejea moja, ambayo ingepasa kuwa muhimu kwa kila Kadiani ambayo vile vile ni mashuhuri katika zilizokosekana katika orodha hiyo, ni ipi hiyo? Ni ile inayotokana na vitabu vyake mwenyewe Mirza Ghulam Ahmad. Orodha hiyo hapo juu mara kwa mara hunukuliwa katika maandiko Ahmadiyya kuhalalisha tafsiri yao potofu ya aya ya Qur'an inayoeleza kwamba Muhammad(s.a.w) ndiye mwisho wa Mitume wa Allah.
Udanganyifu wa 3 wa Kadiani- Tafsiri pekee inayo ya Khatam inayopatikana katika Kamusi la Mirza
Neno Khatam, limetolewa mifano zaidi ya 40 na Makadina lakini hakuna hata mfano mmoja unaotolewa kutoka katika vitabu vya Mirza Qadian. Haishangazi kama utakavyoona kurasa za mbele. Waulizwe Makadiani Mirza alikuwa na maana gani kwa neno Khatam? Hii ni muhimu sana kwa sababu tangu hapo Mirza ambaye hakubaliki na Umma wote wa kiislamu kwa kule kuikana kwake Tafsiri ya Neno Khatam kama ilivyotolewa na Mtume Muhammad(s.a.w)
Tunapoviangalia vitabu vya Mirza Qadian, tunakutana na nukuu ambazo zinaweka wazi jinsi Mirza alivyoilewa maana ya Neno Khatam:
Khatam ul Walad Anbiya- mtoto wa kiume wa mwisho
“Mimi nilikuwa Khatam ul Walad(muhuri wa watoto) kwa baba yangu, hapana mtoto mwengine aliyezaliwa baada yangu”(Braheem Ahmadiyya sehemu ya tano, Roohan Khazain, juzuu ya 212 uk. 113).
2. Khatam ul Anbiya- Mtume wa mwisho
“Baadhi ya bishara katika vitabu vya awali vya Mwenyezi Mungu kuhusiana na Nabii Issa zinafanana na na bishara (ya kuja Mirza) ambayo Mayahudi hawataikubali. Kama ilivyotajwa katika Injili kwa rejea ya bishara hizi kwamba lile tofali walilolikataa kwa hakika ndilo tofali lililo muhimu zaidi, hivyo kwamba yeye (Issa Ibni Maryam) alikuwa Khatamu ul Anbiyya kwa Mitume wa wana wa Irail..... vivyo hivyo ndivyo Mungu alivyoniambia kwamba wanakukana wewe lakini nitakufanya wewe Khatamul Khulafa.(Braheen Ahmadiyya sehemu 5, Roohan Khazain juzuu. 21 uk.267).
3. Khatam ul Khulafa- mwisho wa Mkhalifa.
“Kiroho mimi ni Khatam ul Khulafa katika Uilsmu, kama alivyokuwa Masihi Ibni Maryam yeye ni Khata ul Khulaf katika mlolongo wa Mitume wa Kiyahudi.(Kishtee Nooh, Roohan Khazain juzuu 19.uk17).
“Nukuu kutoka vitabu vya Mirza Ghulam Ahmad, zinathibitisha kwamba neno Khatam Mirza Ghulam lina maana mwisho au mwisho au chochote ambacho kilichopigwa muhuri. Je hii ndio sababu ya wao kupuuzia na ndio kuoziondoa kimya kimya kunakolenga kuwazuga watu au kutoyafahamu maandiko ya Mirza? Unaachiwa wewe msomaji uamue.
Udanganyifu wa 4-Mirza adai kuwa yeye ndiye mwisho wa Mitume.
Suala ni kwamba kwa nini maana ya neno moja imekuwa ikibadilika inakuja kuelezea Khatam un Nabiyyin? Na kwa hakika iwapo maana ya neno Khatam un Nabiyyin ni kwamba Mitume zaidi watakuja kwa idhinisho na muhuri wa Mitume, kwa hiyo neno Nabiyyin kwa mujibu sarufi ya kirabu maana yake lazime kuwepo walau mitume watatu zaidi. Lakini maandiko ya Mirza Ghulam yanatupa taarifa nyingine:
Abarikiwe yule anayenitambua mimi. Katika njia zote za Mwenyezi Mungu mimi ndiye njia ya mwisho, katika mianga yake yote, mimi ndiye mwanga wa mwisho. Bahati mbaya yule anayenitelekeza, kwa sababu bila ya mimi kote ni giza”.(Kashti -i-Nuuh, Roohani Khazain, juzuu ya19, uk. 61 kilichoandikiwa na Mirza).
Jarida rasmi la makadiani liliandika:
“Nukuu hizi zinathibitisha kwamba kwa ajili ya Masihi aliyeahidiwa hapana mwingine anayeweza kuwa Mtume baada ya Mtume(s.a.w) ila ni mtume mmoja tu aliye wa lazima na kuja kwa mitume wengi kutatia dosari busara ya mpango wa Mwenyezi Mungu.”(Tasheed ul Azhan, Qadian, Na. 8, juzuu ya 12, uk.11 tarehe Agosti 1917).
Ni wazi kwamba maelezo haya potofu juu ya neno Khatam, hayana maana ya mwisho bali muhuri, yalikuwa yamefungua mlango wa utume, na kwa kupitia upenyo huu Mirza yeye huyo kwa mara nyngine akaufunga. Kwa maneno mengine, Mirza ameona haya alijaribu kuiba taji la Khatama un Nabiyyin kutoka kwa Mtume(s.a.w), yaweza kuwa kejeli mbaya kwa Mtume(s.a.w).
Kwa kweli jambo hilo ni baya zaidi kuliko unavyoweza kuhisi. Si suala la kudai utume tu. Mirza hakudai utume tu bali alifanya dhambi mbaya zaidi kuliko hiyo kama utakavyoona hako mbele.
Udanganyifu Na. 5-Nani Mirza Qadian
Kila Qadian atasema kwamba, anaamini Khatam Nabiyyin, kwamba anamtambua Muhammad(s.a.w) kuwa ni Miwsho wa Mitume, lakini bado atamtambua Mirza kama naye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Huu ni udanganyifu au huku ni kuvurugikiwa au ni kujichanganya kikauli? Au kipo kilichojificha ambacho hatukioni? Hebu tuchambue kauli hii.
Hebu ifahamike kwamba mfuasi muaminifu wa Mirza Ahmad Kadian lazima akitii kile kilichosemwa na kuandikwa na MIrza, imani yake inapaswa kuwa imani ya inayoelezwa na maadniko ya Mirza, bila ya kujali kuwa yeye kasoma vitabu hivyo au la. Kadian hawezi kuwa na imani inayojikanganya na maandiko ya Mirza. Iwapo hakubaliani na mafundisho yake ajikute kuwa si mkweli katika imani hiyo ya ‘Uislamu’ hivyo ni bora awakane Mirza na Jamaat yake. Hawezi kupanda majahazi mawili tofauti. Akisema hivi basi ni vyema ionekane sasa Mirza ana maana gani katika hiyo Khataman Nabiyyin.
Mirza amedai kuwa yeye ndiye Muhammad
Wahyi wa Mirza unatufahamisha ifuatavyo:
“Muhammad Rasuulullah wa Laziina ma’ahoo ashiddahuu alal Kuffari Ruhamahuu baina hum’ katika ufunuo huu Mwenyezi Mungu ameniita mimi Muhammad na vile vile mjumbe(Roohan Khazain juzuu 18 uk. 207).
Yeyote anayenitofautisha mimi na Mustafa(s.a.w), hakuniona mimi na hanitambui”(Roohani Khazain juzuu 16uk.171).
Mirza adai kuwa yeye ni Khatam ul Anbiyya.
Nimekuwa nikisema kuwa kwa mujibu wa aya “Waakhariina minhum lamma yalhaquu behim na wengineo miongoni mwao ambao hawajaungana nanyi(Qur’an 62:3) katika aina ya Borooz( iliyotafsiriwa na Makadiani kuwa ni taswira, nakala halisi) mimi ni yule yule Mtume, Khataman ul Anbiya(mwisho wa Mitume). Na miaka ishirini iliyopita Mwenyezi Mungu ameniita mimi Muhammad na Ahmad katika Braheen Ahmadiyya, na kutangaza kwamba mimi ni Mtume mtukufu. Kwa hivyo utume hakuna namna yoyote unagongana na hadhi ya Mtume mtukufu(s.a.w) kama ni mwisho wa mitume kwa sababu kivuli hakiwezi kutengwa na umbile asilia. Kwa kuwa mimi ni Muhammad ni kivuli, hivyo njia hii ya muhuri wa mwisho wa mitume unavunjiliwa mbali kwa sababu utume wa Muhammad unabaki na Muhammad”.(Mirza Ghulam katika Ek. Ghalti ka Izala, Roohan Khazain juzuu ya 18, uk.212).
Utume ulifikia mwisho kwa Mtume wetu(s.a.w). Kwa hiyo baada yake hakuna Mtume isipokuwa yule ambaye ameng’arishwa na mwanga wake na yule ambaye amefanywa mrithi na Mwenyezi Mungu. Jueni kuwa umwisho alipewa Muhammad(s.a.w) tangu mwanzo na kisha baadaye akapewa(Mirza) ambaye alifundishwa na roho na kufanywa kivuli chake. Kwa hivyo amebarikiwa yule ambaye amefundisha na amebarikiwa yule ambaye amejifunza(Mirza). Kwa hivyo Mwisho wa Utume ulikadiriwa kuwa Milenia sita ambayo ni siku ya sita katika masiku ya Mwenyezi Mungu....Kwa hivyo Masihi aliyeahidiwa alizaliwa katika Milenia ya sita”.(Zamima Khutba Ilhamiah, Roohani Khazain juzuu ya 16uk 310).
Mirza adai yeye ni nakala halisi ya Muhammad(s.w)
Walakin Rasuulallah wa Khaataman Nabiyyin, katika aya hii kuna utabiri uliojicha hapa ambao ni kwamba kuna muhuri unaohusiana utume mpaka siku ya hukumu, na isipokuwa kwa nakala halisi amaye ni yeye, hapana yeyote mwenye uwezo wa kufungua lango la eleimu iliyojificha kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ka walivyokuwa Mitume; na kwa vile huyo nakala halisi wa Muhammad amabye ni yule Masihi aliyeahidiwa tangu zama za awali, ni mimi kwa hiyo utume ni nakala aniliyopewa. Sasa ulimwengu mzima hautasiaidia mbele ya utume huu kwa sababu kuna muhuri wa Manabii. Mtu anayefanana na Muhammad kwa sifa zote ameshatokea. sasa mbali ya dirisha hilo hakuna dirisha lingine liliachwa kunywewa maji ya Utume".(Aik Ghalti ka azala, Roohan Khazain juzuu ya 18 uk. 215).
Mirza adai yeye ni Muhammad aliyekuja kwa umbile lingine
"Nilipokuwa ni yule Mutme aliyekuja kwa umbile lingine na nilipokamilisha yale yote ya Muhammad ikiwa ni pamoja na Utume unaojiakisi kwa kioo cha kivuli changu, hivyo ni nani huyo anayeweza kudai utume akiwa mtu mwingine"(Ek Ghait Ka Izala, uk.8 Roohan Khazain, vol 18,uk. 212).
"Mwenyezi Mungu amenipa mimi neema ya aliyompa Mtume Mtukufu na akanifanya mimi mkamilifu na amenifanya kuwa mwenye huru na mpole kama aliokuwa na Mtume, kiasi kwamba taji langu limekuwa hasa taji. Hivyo yule ambaye ataungana nami katika Jamaat kwa hakika atakuwa mmoja wa masahaba wa wa mkuu wangu ambaye alikuwa mmbora kuliko Mitume wote. Hafichiki kwa wale wenye uwezo wa kufikiri kwamba hii ndio maana ya neno lile la"wengine miongoni mwao" Mtu anayenitofautisha mimi na Mustafa(Muhammad(s.a.w) hatakuwa ameniona mimi wala hanitambui".Khutbah e Ilhamiah, Roohan Khazain, juzuu ya 16, uk 258-259).
Mirza amedai kuwa yeye ni mbora kuliko Mtume(s.a.w).
"Ukweli ni kwamba kiini cha kuja katika umbile jingine la Mtume mtukufu mwisho wa milenia ya sita(zama hizi katika sura ya Mirza), kina nguvu zaidi, kikamilifu zaidi na chenye msukumo zaidi kuliko zile zama za awali, ni sawa na usiku wa mbalamwezi ya mwezi 14 mng'aro(Khutba i Ilhamiyah, Roohan Khazain, juzuu 16 uk 271-272).
Utukufu wa Mtume wetu(s.a.w) ulionekana miaka elfu 5 ukiwa sawa na sifa zake na kipindi hicho hakikuwa kilele cha mandeleo ya kiroho. Kilikuwa hatua ya mwanzo kuukwea mnara mrefu wa ukamilifu wake. Baada ya hapo kumea huko kiroho kwenyewe kulifikia haiba yake kamili mnamo miaka alipozaliwa Qadian wakati huu"(Mirza in Khutba i Ilhamiyya, Roohan Khazain, vol 16, uk 266).
Mirza ameingizwa katika Kalima ya Shahada
Pamoja na kuja Masihi aliyeahidiwa imetokea tofauti moja(katika maana ya Kalima) imetokea na hiyo ilikuwa kabla ya kuja Masihi, katika maana ya Muhammad Rasuulullah nyakati hizo ilikuwa wakitajumuishwa na mitume, lakini alipokuja Masihi aliyeahidiwa, Mtume mmoja zaidi ameongezwa katika maana Muhammad Rasuulullah...kwsa hiyo katika kuingia Uislamu bado ni Kalima hiyo, tofauti moja tu ni kwamba kuja kwa Msihi aliyeahidiwa kumemuongeza Mtume mmoja katika maana yake...zaidi, hata kama tutakubali kwa kujaalia kutokuwezekana kwamba jina takatifu la Mtume(s.a.w) kwamba limejumuishwa katika kalima tukufu kwasababu yeye ni mwisho wa Mitume hata hivyo hapana haja na hatuhitaji kalima mpya kwa sababu Masihi aliyeahidiwa si mtu anayeweza kutenganishwa na Mtume mtukufu, kama yeye(Mirza) mwenyewe alivyosema: "Umbile langu ni lile hasa umbile la Muhammad Rasuulullah". Vile vile, "yule anayenitenganisha mimi na Mustafa hatakuwa ameniona mimi wala hanitambui. Na hoja yake hapa ni kwamba Mwenyezi Mungu ameahidi kwamba atamleta katika umbo lingine "Khataman Nabiyyin" katika ulimwengu huu kwa mara nyingine zaidi kama Mtume kama ushahidi unaotokana na "Na wengine miongoni mwao"... Kwa hivyo Masihi aliyeahidiwa(Mirza Qadian) yeye mwenyewe ni Muhammad rasuulullah, ambaye ameletwa kwa umbo lingine katika ulimwengu kueneza Uislamu. Kwa hiyo hatuhitaji kalima yoyote mpya. Ingawa, kalima mpya ingekuwa lazima iwapo baadhi ya watu wamepewa umbo lingine badala Muhammad Rasuulullah. Kwa hiyo zingatia"(Kalimatul Fasl, ukالصفحات [1] [ 2]