Bismillah Al-Rehman Al-Raheem
Anti Ahmadiyya Movement of Islam
Tatizo la ukadiani
(Na Sayid Abu’l Ala Maudud)
Wanazuoni wa Kiislamu wakiwakilisha jumuiya na vyama vya Kiislamu kutoka sehemu zote za Mashariki na Magharibi ya Pakistan walifanya Mkutano mjini Karachi kujadili maoni na mapendekezo ya serikali juu ya katiba mpya iliyowasilishwa Bungeni.
Mkutano huo ukamalizika kwa maoni na mabadiliko mengi (ya katiba) ambapo mojawapo ni; “…tunataka serikali iwahesabu wale wote wanamuamini Mirza Ghulam kama kiongozi wa dini kuwa ni jamii ya watu wachache sawa na jamii nyingine nyingi za watu wachache wasio waislamu nchini na iwape kiti kimoja katika Bunge la Punjab.”
Maoni mengine yalikuwa ni mazuri na ya wazi mno kiasi kwamba maadui hawakuweza kuyashambuliya, na pale waandishi wakorofi walipofanya hivyo, ushawishi wao haukuwa na maana miongoni mwa Wasomi.
Idadi kubwa ya Wapikistani wasomi hawakushawishika kuwa maoni yaliyotaka kutengwa kwa Makadiani yalikuwa ya busara na muhimu. Lakini hapa mimi nitafafanuwa kinagaubaga kwa nini wanazuwoni wote wa Kiislamuwalikubaliana kuyatetea kwa pamoja maoni haya.
Kuwa jamii ndogo huru isiyo ya kiislamu ni jambo ambalo kiada na kimantiki, makadiani walilitaka wenyewe. Wao ndio waliosababisha na kusisitiza kila jambo ambalo limewapelekea kuwa jamii ya watu wachache wasiowaislamu.
Kwanza kabisa ni ule upotoshaji wao wa maana ya “Mwisho wa Mitume” ambayo kwayo wametofautiana na Waislamu wote wanaomuamini Muhammad (s.a.w) kama Mtume wa Mwisho na kwamba hakutakuwa na Mitume baada yake hadi siku ya hukumu.
Hii ndiyo maana ambayo Maswahaba wa Mtume waliielewa na ndiyo maana inayotokana na aya hii “Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali yeye ni Mtume wa Mungu na Mwisho wa Mitume” (33:40)
Maswahaba wa Mtume waliwapiga vita wale wote waliojifanya manabii baada ya kutawafu Muhammad (s.a.w). Na hii ndiyo maana ambayo Waislamu waliielewa kutoka vyanzo vyote, na ndio kusema hawakumkubali na hawamkubali yeyote anayejifanya nabii.
Kwa mara ya kwanza katika historiya ya Waislamu, Makadiani peke yao ndio waliotafasiri aya ya Qur’an, “Mwisho wa Mitume kuwa eti ina maana kuwa Muhammad ni Muhuri wa Manabii ambao unasadikisha na kusainisha utume wa Manabii wengine. Hiki tunachokisema chaweza kuthibitishwa na maandiko yaliyonukuliwa hapa kutoka katika vitabu na maandiko ya Makadiani. Hizi ni nukuu tatu.
· “Kristo (a.s) aliyeahidiwa alisema hivi katika tafsiri yake ya ‘Khatamu Nabiyiin’: maana yake hapa ni kwamba hakuna ujumbe wa Nabii unaoweza kuidhinishwa na kuthibitishwa isipokuwa kwa muhuri wa Muhammad. Kama vile kila waraka usivyokubalika isipokuwa mpakauthibitishwe kwa muhuri na saini, kwa hiyo kila ujumbe ambao hauthibitishwi na muhuri wa Muhammad si wa kweli. (Malfuzal Ahmadiya edited by M. Manzur Ilahi pp.290)
· “Hatukanushi kuwa Muhammad (s.a.w) alikuwa komeo la Manabii, lakini wanachokielewa watu wengi kinapingana na utukufu wa Mtume (s.a.w) kwani kinapelelekea katika imani kuwa Mtume amelinyima Taifa lake neema kubwa ya Allah- Manabii.
· “Maana ya aya hii ni kwamba Mtume ni muhuri unaothibitisha ujumbe baada ya ule wake, hivyo hapatakuwa na Nabii iwapo hatothibitishwa na Mtume mtukufu Muhammad. Maana hii tu ndiyo tunayoikubali sisi”. (Al-Fadl, 22 Septemba 1939).
· “Saini ni muhuri, na kama Mtume mtukufu ni muhuri,yawezekanaje basi pasiwepo na manabii wa kuthibitishwa.” Al-Fadl,22 Septemba 1923).
· Tofauti baina ya Waislamu wote na Makadiani haziishii tu katika ufafanuzi au upotoshaji wa neno “Khatama”, bali tofauti zilikuwa kubwa zaidi kwani ukadiani ulidai dhahiri shahiri kuwa si nabii mmoja tu anaeelekea kutokea baada ya Muhammad (s.a.w) bali ni maelfu ya Manabii. Hili limo katika maandiko ya kadiani, baadhi yake ni haya yafuwatayo, “Kutokea kwa manabii wengi wapya ni jambo linaloonekana wazi kama juwa wakati wa mchana.” ( The reality Of Qadianism by Mirza Bashir Mahmud pp.228)
· “Wailamu wanadai kimakosa kuwa wahai wa Allah umekoma na hakuna tena manabii watakaotokea. Hawamdhanii Mungu kwa haki. Kwangu mimi, nasema kuwa sio tu nabii mmoja atakaetokea bali maelfu.” Anwar Khilafat by Mirza Bashir Mahamud pp 62)
· “Kama mtu angenowa mapanga jirani na shingo yangu kunitishia akinitaka niseme kuwa hakuna nabii atakayetokea baada ya Muhammad (s.a.w) ningemwambia, wewe ni muongo, ni kweli, lazima wawepo manabii baada yake” (Ibid pp. 65)
Baada ya Ghulam kufunguwa njiya ya wahai na Manabii, akadai kuwa yeye ni nabii. Makadiani wakaliamini dai lake na wakalikubali kabisa. Tunanukuu hapa baadhi ya matamshi na maneno ya kuthibitisha upotofu na uzushi na mengineyo yawayo.
· “Kristo aliyeahidiwa alitangaza dai lake la kupata Utume na kuwa nabii, kama alivyoandika Mimi ni nabii na Mtume’ (AlBadr 5 Mar 1908), au kama alivyoandika pia ‘mimi ni nabii kwa maamrisho ya Allah. Nikilikataa hili basi mimi ni muwovu. Na kama Allah ananiita hivyo iweje mimi nikatae. Nitalitimiza jambo hili hadi kufa kwangu’ (Letter to Akhbar Am by Mirza Ghulam Ahmad iliyoandikwa siku tatu kabla ya kifo chake na kuchapishwa tarehe hiyohiyo ya kifo chake yani, Mei 26 1908)
· Sifa ambazo Uislamu unazitowa kwa Kristo aliyeahidiwa maanake ni kuwa kweli yeye ni nabii.” (The Reality Of the Message by Mirza Bashir pp.174)
Kipengele kimoja cha msingi cha watu wanaodai kuwa ni Manabii ni kile cha kuwapachika ukafiri wale wasiomuamini. Hivi ndivyo wasemavyo Makadiani katika hotuba zao za hadhara na katika machapisho yao dhidi ya Waislamu wanaopinga dai lao. Nanukuu yafuatayo kutoka katika hotuba zao:
· “Waislamu wote asiokula kiapo cha utii kwa Mirza Ghulam ni Makafiri hata kama hawajalisikia jina lake” ( Ayina Sadakat by Mirza Bashi Eddin pp.35)
· “Mtu yeyote anayemuamini Musa na asimuamini Yesu Kristo, anayemuamini Muhamad lakini asimuamini Ghulam Ahmad sio tu ni kafiri,bali yuko katika kiwango kikubwa mno cha ukafiri.” (Word Of Dermacation by Bashir Ahmad pp 110).
· Kwa kuwa tunamuamini Mirza Ghulam Ahmad kama nabii, na wale wote wasiokuwa Ahmadiya hawamuamini, basi sisi tunawahesabu wale wasiokuwa kadiani kuwa ni Makafiri kwa mujibu wa aya ya Qur’an isemayo kuwa kutomuamini nabii mmoja ni kuwakataa manabii wote.” (Mirza Bashir Ahmad’s article in Al-Fadl Mei 26, 1922)
Makadiani sio tu wanasema kuwa wao wanapingana na Waislamu kwa kuamini ujumbe wa Mirza bali wanasema kuwa hakuna cha kuwanasibisha wao na Waislamu kwani Mungu wao, Uislamu wao, Qur’an yao, Sala yao na funga yao ni tofauti na Waislamu.
-Hotuba ya Khalifa wa Kadiani iliyochapishwa katika Al-Fadl,
Agosti 21, 1927 chini ya kichwa Advice for Students’
kinawafafanulia wafuwasi wake tofauti kati ya Ahmadiya na
wasio Ahmadia. Anasema “... Kwa kuwa Kristo aliyeahidiwa
alisema kuwa. Uislamu wao, Mungu wao na hija yao ni
tofauti na zetu, daima tunatofautiana nao kwa killa kitu.”
Mnamo Julai 30,1931 Al-Fadl likachapisha hotuba nyingine ya Khalifa wa Kadiani ambapo alielezea ugomvi uliotokea baina ya Makundu mawili. Moja likatowa hoja kuwa kwa vile tofauti kati ya Makadiani na Waislamu zinajulikana, na Kristo aliyeahidiwa amekwishazifafanuwa hakuna haja ya kuanzisha shule binafsi za kadiani: tunaweza kuyasoma yale mambo yote yasiyo na ubishani katika shule za Waislamu. Makundi mengine yakakataa. Huku bado wakibishana, Kristo mwenyewe aliyeahidiwa akaingia na kusikiliza mabishano yao. Kisha akatowa hukumu hii, akisema: “Ni makosa kusema kuwa tunatofautiana na Waislamu katika suala la kifo cha Yesu tu. Tunapingana nao katika yote; Mungu, Mtume (s.a.w), Qurian, sala, hija na zaka. Kwa kifupi aliwafafanulia kuwa tunatofautiana kabisa na Waislamu kwa mambo yote yanayohusiana na dini”.
Makadiani wenyewe ndio waliovunja mahusiano na Waislamu kwa lile pengo kubwa waliweka baina yao na Waislamu. Walijikusanya peke yao kana kwamba walikuwa ni jamii ndogo isiyo ya kiislamu kama inavyothibitishwa na maandiko yao wenyewe.
· “Kristo aliyeahidiwa aliweka wazi kuwa Ahmadiya wasisalishwe na waislamu katika sala. Baruwa nyingi zinakuja kuulizia jambo hili. Jibu langu kwao wote ni kuwa hata mkirudia swali hili mara ngapi mimi nitajibu kuwa si sahihi, si sahihi, si sahihi kusalishwa na mtu asiyekuwa Ahmadiya.” (Anwar Khilafat by Mirza Bashir Mahmud pp. 89)
· “ Wala tusiukubali Uislamu wa wale wasiokuwa kadiani, wala tusisalishwe nao kwa sababu kwa maoni yetu wao si waumini (kwani) hawamuamini mmoja wa Manabii wa Allah.” (Ibid. Pp. 90)
· “Anapokufa mtoto wa asiyekuwa Ahmadiya kwa nini hatumsalii ilihali yeye hapingi kuwa Mirza Ghulam ndiye Kristo aliyeahidiwa! Mimi binafsi nawauliza wale ambao wameniuliza kwa nini sisi hatumsalii mtoto wa Muhindu au Mkristo pale wanapokufa.... Mtoto wa asiyekuwa ahmadiya ni mmoja wa watu wasiokuwa Ahmadiya na kwa sababu hii kuwasalia ni makosa.” (Ibid. Pp.93).
· “Kristo aliyeahidiwa alichukizwa na Ahmadiya aliyetaka kumtowa binti yake kwa mtu asiyekuwa Ahmadiya. Mtu huyo alimuomba mara nyingi lakini Kristo aliyeahidiwa akamuamuru asifanye hivyo. Baadae mtu huyo akaidhinisha ndowa ya binti yake baada ya kifo cha Kristo aliyeahidiwa basi Khalifa akam*****uza kutoka kwenye nafasi yake ya kidini na hakuikubali toba ya mtu huyo japo alirudiya mara nyingi hata ikapita miaka sita.” (Ibid. pp. 93-94)
- ENDELEA
· “Kristo aliyeahidiwa hakuruhusu shughuli yoyote na Waislamu isipokuwa wale walioruhusiwa kufanya shughuli na Wakristo na Wayahudi. Alitutenganisha na waislamu katika sala, akazuia mahusiano nao ya ndowa, na kusalia maiti zao, sasa nini tena cha kutunasibisha nao? Mashirikiano na watu yanategemea mambo mawili na yana matapo mawili, mambo ya kidini na ya kiduniya. Njiya kuu ya mashirikiano ya kidini ni kusali kwa jamaa na kuowana. Mambo haya mawili yanakatazwa katika dini yetu, na mkisema tunaruhusiwa kuoa mabinti wa kiislamu, mimi nasema hili linahusu Wakristo pia. Na kama mkiniuliza mbona ni halali kuwasalimu Wasio Ahmadiya, jibu langu litalingana na Hadith sahihi ya Mtume. Yeye aliwarudishia salamu Mayahudi”. ( Word Of Demarcation published in Rioy av Religinter, pp. 69).
Sio tu Makadiani walivunja mahusiano na mashirikiano na Waislamu kwa hotuba na maandiko yao, bali walifanya hivyo kwa vitendo kama mamia kwa maelfu ya waislamu walivyoripoti. Walijiundia jamii ya peke yao wakikataa kusali au kuowana na Waislamu.
Ikiwa tatizo ndilo hilo, hakuna mantiki kwa Makadiani kubakiya kuwa sehemu ya jamii ya Waislamu. Si lazima kwamba uhuru wao utolewe kisheriya kwani jambo hilo limekuwepo kwa miyaka hamsini iliyopita
Kwa ule mwenendo wao, Makadiani wamethibitisha kile ambacho kilikuwa kigumu kuthibitika hapo kabla kuhusiyana na hikima na faida za kukoma kwa ujumbe wa Allah. Huko nyuma mtu alikuwa akijiuliza kwa nini wahayi na Mitume wamekoma kuja
Hivi leo, uzowefu umeonesha Hikima kubwa na faida za neema hii ya Allah. Imani kuwa Muhammad ndiye Mtume wa mwisho iliwaunganisha waumini wote katika kumfuwata Mtume mmoja tu, na hivyo imani hiyo ikawajengeya nguvu, umoja na mashirikiyano. Kuibuka kwa itikadi ya manabii wengi kunalimegamega Taifa katika makundi mengi ya kijamii.
Tukiwa*****uza Makadiani hakuna mtu yeyote miyongoni mwetu atakayethubutu kusimama na kudai utume kutuvurugiya umoja na mshikamano wetu. Lakini kama tutaufumbiya macho Ukadiani, basi tutawasaidiya na kuwahamasisha wazushi wengi kuibuka na kudai hivyo, na hivyo tutakuwa tumeshiriki katika kuuhujumu mshikamano wetu.
Na tukiipuziya hatari hii, mfano wetu utaigwa na vizazi vyetu, na kwa hivyo hujuma hii haitakoma na jamii yetu itakabiliyana na hatari za aina nyingine kila siku; hatari hizo zitaligawa Taifa letu.
Hii ndiyo hoja yetu sahihi ambayo kwayo tunaegemeza madai yetu ya kuwafanya Makadiyani kuwa jamii ya watu wachache yenye haki za jamii ndogo za Wasiowaislamu. Kwa hakika hoja yenye nguvu ni hii yetu na hakuna hoja nyingine yenye mashiko inayoweza kutolewa dhidi ya dai letu.
Wale wanaopinga dai letu wanataka kuwababaisha watu kwa vijisababu na vipingamizi visivyohusiyana kabisa na suwala hili. Mathalani eti wao wanasema kuwa makundi mbalimbali ya Waislamu bado yanashutumiyana kwa ukafiri. Na kama tutaendeleaya kulitenga kundi moja baada ya jingine Taifa litatoweka.
Aidha wanasema kuwa yapo madhehebu huru ya Kiislamu kama Ukadiani, ingawaje hayatofautiyani na Waislamu kiitikadi. Eti wanatuhoji iwapo hayo nayo tunakusudiya kuvunja mahusiyano nayo au tuamuwe tu kuwachukuliya Makadiani kama madhehebu hayo bila chuki na hasama.
Watu wengine wengi walihadaiwa na wito wa Makadiyani wa kuingiya katika Uislamu. “Makadiani wanateteya Uislamu dhidi ya mashambulizi ya Wakristo na Waaryan, na hivyo wanaueneza duniyani kote, ni vyema kuwachukuliya hivyo.” Lakini sisi tutazungumziya kila nukta kati ya nukta hizi ili kujibu swali lolote linaloweza kujitokeza.
Kweli inasikitisha kuwa makundi mbalimbali ya Waislamu yanashutuyana kwa ukafiri lakini si sahihi kulifanya hili kuwa kisingiziyo cha kuuhesabu Ukadiani kuwa ni dhehebu halali la Kiislamu; hii ni kwa sababu: - a) Hakuna mantiki kutowa mifano ya shutuma mbaya na kuhukumu kuwa kila shutuma isikubalike, na kwamba kumshutumu mtu yeyote kwa ukafiri si sahihi. Kwa kweli ni makosa kuwashutumu watu kwa ukafiri kwa khitilafu ndogondogo kama ilivyo makosa kuukubali upotevu uliothibitika wazi wazi wa kutoka katika misingi ya Uislamu. Wale wanaofikiya hitimisho kutokana na shutuma zisizo za kweli dhidi ya wanazuwoni fulani kwamba aina zote za shutuma si sahihi wanaombwa kujibu iwapo Muislamu atabakiya kuwa muumini pale napodai yeye ni Mungu au Mtume, au iwapo anatoka katika mafundisho ya msingi ya Uislamu.
- b) Makundi na Madhehebu ya Kiislamu yanayotoleyana shutuma ambazo zinatumika hapa yalifanya kongamano Mjini Karachi na yakakubaliyana juu ya kanuni za msingi za dola ya kiislamu. Yalikubaliyana juu ya kanuni hizo kwa sababu kila moja linaliona kundi au dhehebu jingine kuwa ni la Kiislamu. Hakuna hata moja lililoliyona jingine kuwa nje ya dini japo kulikuwa na tofauti ndogo ndogo miyongoni mwao. Hivyo kudhani kuwa kuutenga ukadiani kutoka katika Taifa la Kiislamu kutakuwa chanzo cha kuyatenga mengine mengi ni njozi tu.
- C) Shutuma ya jamii ya Kiislamu ya kuwashumu Makadiani kwa ukafiri si sawa na shutuma dhidi ya wengine. Makadiani, kwa uzushi, walidai kuwa kuna Mtume mpya ambaye anawahesabu wale wanaomuwamini yeye kuwa ni jamii tofauti na kuwaona Makafiri wale wasiomuwamini. Kwa hiyo Makadiani wote wanakubaliana kuwashutumu waislamu kwa kukufuru na Waislamu nao piya wamewahukumu Makadiani kuwa ni Makafiri.
Hivyobasi, inadhihirika wazi kuwa hii ni tofauti ya kimsingi ambayo haiwezi kuchukuliwa kuwa ni ndogo kama zilivyo tofauti ndogo ndogo- miongoni mwa mdhehebu ya Kiislamu.
Bila shaka kuna madhehebu mengine ukiondowa Qadiani ambayo yamepinzana na Waislamu na kuvunja uhusiyano nao, na kujiundiya madhehebu zao peke yao, lakini kosa ambalo hawa wamelifanya ni tofauti kabisa na lile lililofanywa na Makadiyani kwa namna nyingi. a) Madhehebu haya yakajitenga kabisa na jamii ya Waislamu kiyasi kwamba yamekuwa kama upukupuku njiyani ambao haudhuru wala haudhuriki. Kuwepo kwao kwaweza kustahamilika. Makadiyani huchanganyika na Waislamu, wakijidai kuamini mafundusho yao, wakiyajadili na wengine na kubishana kwa jina la Uislamu, na kwa kweli, huigawa jamii ya Waislamu na kuwateka upande wao. Mtafaruku mkubwa, mfarakano wa kufedhehesha na tawala kandamizi zimewasibu Waislamu kutokana na Ukaragosi wa makadiani kwa nchi za kigeni. Kwa sababu hii na kwa sababu nyinginezo hatuwezi kuvumiliya kukaa na Watu hawa.
b) Madhehebu ambayo yana tofauti na jamii ya Waislamu yanahukumiwa na sheria ya Kiislamu. Sheria inahukumu iwapo hizo imani zao binafsi zinawatowa nje ya dini. Na hata tukijaaliya kuwa wao si wafuwasi wa Uislamu , imani yao haitawatiya hatarini Waislamu na haitasababisha matatizo ya yoyote ya kijamii, kiuchumi na kisiyasa. Lakini uzushi wa Makadiyani unahatarisha imani ya mamiya kwa maelfu ya Waislamu na kusababisha tatizo la kijamii katika kila familiya ya kiislamu inayoshawishika nao kiyasi kwamba mume humwacha mkewe, baba hutengana na mwana, na uwadui hutokeya baina ya ndugu. Zaidi ya hivyo madhehebu mengine yasiyokuwa Kadiani hayana malengo yoyote ya kisiyasa ambayo yangeweza kuonekana kama hatari kwa maisha yetu ya kijamii. Lakini makadiani wanazo nyendo fulani hatari za kisiyasa ambazo haziwezi kufumbiwa macho.
Makadiani walikuwa na uhakika kabisa kuwa katika jamii huru ya Kiislamu, huo utume unaodaiwa usingeliweza kushitadi au kufikiya malengo yake. Wao wanajuwa kuwa jamii ya kiislamu inachukizwa na madai kama hayo kwani yanawaparaganyisha Waislamu, yanavunja sheriya ya kiislamu na yanaimegamega jamii ya Waislamu.
Huku wakifahamu msimamo wa Maswahaba wa Mtume katika kuwakabili wazushi wa Utume , na huku wakiutambuwa ukweli kuwa pale Waislamu wanaposhika madaraka katika nchi yoyote katu hawaruhusu madai ya uzushi, Makadiani wakaamuwa kujinasibisha na serikali ya kikafiri kwa sababu hakuna mazingira mengine wanamoweza kuuhujumu Uislamu kwa uzushi.
Wameiteka Jamii ya Waislamu kwa vile wanawaita katika mafundisho yao kwa jina la Uislamu. Wanajuwa vizuri sana kuwa ni kwa maslahi yao wanaunga mkono utawala wa wageni kwani unawakaba Waislamu na kuwasaidiya wao kupata maslahi yao na kuuhujumu Uislamu. Taifa huru la Kiislamu kwao wao ni adui na halina faida, ni Taifa ambalo wao hawalipendi kabisa.
Twaweza kunukuu maandiko mengi ya Mirza {Madai ya Ahmad na mengine kutoka katika maazimio ya wafuwasi wake} lakini yatosha kunukuu baadhi tu bila sherehe.
· “Serikali ya Mwingereza imetupa mengi mazuri, imetusaidiya na imetupendeleya kiyasi kwamba tukiondoka hapa, si Maka wala Istanbul itakayotupa hifadhi. Sasa basi kwa nini nyie muishuku hisani yake”. (Ahmadiyan Talks, Vol 1 pp. 146).
· “Siwezi kufanya nikitakacho Maka, Madina, Damascus, Persia, Kabul au Roma isipokuwa chini ya hifadhi ya serikali hii ambayo mimi naiombeya utukufu na ushindi kwa Mungu”. (conveying the message by Mirza Gh