عرض المقال :Facts & Figures
  الصفحة الرئيسية » مـقـالات الموقـــع » كشف البلية بفضح الأحمدية » Non - Arabic Articles » Swahili

اسم المقال : Facts & Figures
كاتب المقال: webmaster

Harakati za Ahmadiayya na uzushi wa takwimu

 

Kupindua na kugeuza ukweli na takwimu ilikuwa ndio tabia ya Mirza Ghulam Ahmad, mwasisi wa harakati za Ahmadiya. Mirza alijenga  mazoea ya kucheza na takwimu, akiwa na lengo la kuvuruga ukweli akilenga kuwadanganya wafuasi wake na umma kwa ujumla. Tabia hii haikukomea kwake, imekuwa ikiendelezwa na wafuasi wa kundi hilo hadi hii leo. Kwa miaka kadhaa sasa, Mirza Tahir kiongozi wa Ahmadiya hivi sasa amekuwa akijigamba kuwa na maelfu ya watu wanaojiunga na kundi hilo kila mwaka. Amekuwa akiongeza mara dufu ya idadi hiyo kila mwaka. Kwa mfano mwaka 1998 Mirza Tahir alidai:

 

“Katika kipindi changu cha miaka 16 ya ukhalifa, idadi isiyohesabika ya wafuasi imeongozwa na Mungu kuja katika uahmadiya. Kwa mwaka mmoja tu watu 3,000,000 waliingia uahmadiya, hiyo ilikuwa baraka kubwa ambayo hata zile nchi maarufu haziwezi walau kuota kupokea wageni wa idadi hiyo”.(Kauli aliyoitoa Mirza tahir mamo juni 10, 1998, yaliyochapishwa na Afazl International la juni 26 –julai 2, 1998 uk 4).

 

Katika kauli yake nyingine aliyoitoa tarehe hiyo hiyo na kuchapishwa katika toleo hilo hilo, Tahir alidai:

 

“Kwa wakati huu, Jamaat (Ahmadiya) imejaaliwa na Mwenyezi Mungu kuongezeka na kufikia idadi ya wafuasi milioni 10,000,000 na siku zijazo inatazamiwa kuongezeka zaidi kwa kuwa katika kila mwaka makumi ya milioni huingia Jamaat”.

 

Hivi karibuni Qadiani walidai katika moja ya mijadala iliyohusu uqadiani kuwa idadi yao ilikuwa 10,000,00 mpaka mwaka ”.

Wakitumia tarakimu hizo za uongo, Maqadiani huhoji iwapo wao ni waongo mbona watu wanamiminika kujiunga na uqadiani kiasi hicho.

Kwamba mpaka mwaka 1998 walikuwa wamepata wafuasi zaidi ya milioni 10,000,000. Kwa hiyo Mirza Tahir kiongozi wa kundi hilo la wadanganyifu amekuwa na matarajio kwamba kila mwaka idadi hiyo itakuwa ikiongezeka mara mara  mbili zaidi.

Likitazamwa kwa mazingatio dai hili ni rahisi kuibua maswali mengi, moja wapo je upo uwezekano Ahmadiya kupata idadi hiyo kubwa ya wafuasi katika kipindi cha mwaka mmoja tu. Takwimu hizi zinaingia akilini kweli! Ni labda kwa mtu aliyepunguani anayeweza kukubali majigambo haya ya kiwendawazimu. Ni namna gani mtu huru anavyoweza kuyathibitisha madai haya. Ni vigumu sana kufanya sensa kuwajua maqadiani kwa vipimo vya kimataifa.

Umuhimu wa takwimu

Mirza Ahmad aliahidi kuandika juzuu 50 za Braheen Ahmadiya na akatangulia kuchukua malipo(advance payment). Kutokea mwaka 1880-1884 akaandika juzuu 4 tu. Baada ya juzuu hizo 4, akaacha kuandika mfululizo huo, badala yake akageuka kuandika na kuuza vitabu 80 alivyoviita Roohani Khazain kwa miaka 25. Baada ya hap akarejea kuandika juzuu ya tano ya Braheen-Ahmadiyya kisha katika neno la awali la juzuu hiyo akatahayari kuandika ifuatavyo:

“Awali nilikusudia kuandika juzuu 50, lakini nimelazimika kukomea  juzuu  hizi 5 tu kwa kuwa tofauti ya kati ya namba hizo mbili(50 na 5) ni ile sifuri iliyoko kwenye 50,  kwa ajili hiyo ahadi yangu(ya kuandika juzuu 50) imekamilika kwa kuandika juzuu hizi 5”.

Sambamba na kauli hiyo, akatangaza kuandika kitabu kingine alichokiita Arbaeen kwa kukigawanya katika sehemu sehemu 40. Kama ilivyokuwa katika Braheen, Mirza alipokamilisha kuandika sehemu 4 akaacha kuandika kitabu hicho na kudai:

“Kama Mwenyezi Mungu alivyofanya katika kufardhisha swala alianza na idadi ya 50 akazipunguza hadi kufikia 5 mahala pa 50, vivyo hivyo kwa sunna hiyo ya Mola Karim, nazipunguza juzuu hizo na kuzifanya 4 mahala pa 40”.(Arbaiin N 4. Roohani Khazain juzuu ya 17 uk. 442).

Majigambo kuhusiana na kukua kwa Uhmadiya

Katika kipindi cha uhai wake, Mirza Ghulam alidai katika vitabu vyake mbali mbali kwamba ana mamia ya maelfu ya wafuasi waliochukua ahadi kwake. Kuhusiana na dai hilo aliandika:

“Mwenyezi Mungu ameisheheneza wafuasi wangu miji ya Punjab na India. Kwa mika michache tu zadi ya watu laki moja wamekula kiapo mbele yangu”.(Risala Tohfatun Nadwa, Roohan Khazain juzuu ya 19 uk. 101).

Katika matamshi mengine Mirza alidai:

“Naweza kuapa kwamba watu 100,000 katika Jamaat Ahmadiya wamenikubali mimi kikweli kweli na wanajitahidi kuwa waadilifu na wanaposikiliza hotuba zangu, hutokwa na machozi yanayolowanisha hadi kola za mashati yao”.(Mirza semi za Mirza Ghulam zilizotajwa katika Sira ya Mahdi,  sehemu ya 1uk. 165, riwaya N 157 na Mirza Basheer Ahmad(Mirza Ghulam).

“Mwenyezi Mungu amenitukuza mimi katika nyanja zote. Kwa hivyo ningepaswa kumshukuru mara alfu kwa kuwa  watu 400,000 wameungama dhambi zao  kwangu na wameahidi kuachana na ukafiri.(Tutamma Haqeeqattul Wahi, Roohani Khazain juzuu ya 22 uk. 553).

“Mara zote nimekuwa nikiwashauri kwa hisia  wafuasi wa Jamaat walioko  sehemu mbali katika miji ya Punjab na Hindustan ambao kwa fadhila zake Mwenyezi Mungu, idadi yao inafikia mamia ya maelfu, kwamba wanapaswa  kuyakumbuka mara kwa mara mafundisho yangu niliyoyapandikiza katika vichwa vyao kwa hotuba na maandiko kwa muda wa miaka 26, yanayowaamrisha kuitii serikali hii ya Uingereza”(Matangazo yaliyoitwa “malekezo muhimu kwa wana jamaat wenzangu, mkusanyo wa matangazo I]k,=8juzuu 3 uk. 583).741

Katika gazeti rasmi la propaganda za maqadiani, yametolewa madai ya majigambo. Katika gazeti lao hilo waliandika kama ifuatavyo katika tahariri:

 

“Yaa Masiha Mowood, ujasiri, matumaini na matarajio yako yanadhihirishwa na ukweli huu kwamba kwa mitume wengine wajibu wao ulikuwa kupata tu watu wanaowakubali kuwa wao ni mitume, lakini kwako kulikuwa na ugumu wa namna mbili: Ule wa kukubalika kuwa kuna mtume mwingine atakayekuja na ugumu mwingine ni ule kukubalika kuwa wewe ni mtume. Hivyo umelifanya jambo hili kama nguzo ya imani kwa watu 400,000”.( Gazeti la AlBadri, Qadiani, juzuu ya 8 n 30 uk. 4 tarehe 11n20 mei 1909, Qadian, Qadian Madhab  toleo la 1995 uk 500.

“Baada ya kusoma tamshi hili(lililotajwa hapo juu) hapakuwa na shaka yoyote kwamba 1909 Jamaat ya watu 400,000 walimkubali Masihi Mowood, Hazrat Ghulam kama ni mtume”. (AlFazl Newspaper, Qadian, uk. 11n67uk.67 tarehe 26 februari 1924, Qadian Madhhab toleo la 1995, uk 500).

Aliyekuwa akijiita mtume, mara Masih mara Mahd alitoa matamshi hayo kukonga nyoyo za Wanajamaat la kuchekesha aliyemfuatia, Mirza Basherudii Mahmud, Khalifa wa pili, naye akaiga maneno hayo. Kwa maneno yake Khalifa huyo alidai:

“Naweza kuthubutu kuwaambieni idadi ya wafuasi wa jamaat inakadiriwa kufikia watu 400,000 mpaka 500,000. Kundi la Ghair Mubain la mijini Lahore lina watu 1000 hivi.(Kauli ya Mirza Basheer mbele ya mahakama iliyotajwa katika gazeti AlFazl Qadian tarehe 26 mpaka 29 juni 1922, juzuu ya 9,n 101-102, uk. 6, Qadian Madhhab toleo la 1995, uk 500).

“Sisi Ahmadiya zaidi ya laki 400,000 tunajiandaa kuwapeni mikono(Wahindu) iwapo mtakubali masharti yaliyotajwa  Paigham.(Tangazo la Khwaja Kamaludin, tarehe 15, 1908 lililotajwa katika Paigham Sulh uk.6 Qadiani Madhhab toleo la 1995, uk. 1905.

“Katika kesi ya Akhbar ‘Mubahila, mashuhuda wa Ukadiani wanatajwa kufikia 1,000,000. Mnamo mwaka 1930, kwa mujibu wa Mwandishi wa kijitabu cha ukadiani ‘Kaukab Daree’ alidai kuna zaidi ya Makadiani 2, 000,000 duniani kote. Katika mdahalo uliofanyika mwaka 1932  mjini Bheerah(Punjab), Maulana Mubaraka Ahmad Saheb, Profesa Jamia Ahmadiyya Qadiani, walidai kwamba watu waliokubali ukadiani wanafikia 5,000,000. Hivi karibuni Abdulrahim Dard, mlinganiaji wa ukadiani alitoa matamshi akidai mbele ya Bwana Philby nchini Uingereza kwamba miongoni mwa Waislamu mjini Punjab wengi wao ni Maqadiani,. Punjab ina zaidi ya Waislamu Milioni 15, hii kwa mujibu wa Abdulr Rahiim Dard inamaanisha wapo makadiani zaidi ya 7,5000, katika mji wa Punjab.(Risala Shamsu Islam, Bheera, Punjab, juzuu ya 5 N 10  Madhehebu ya Qadiani toleo la 1995, uk.50).

 

Khawaja Hasan Nizami Saheb alidai kwamba Mian(Mahmud Ahmad, Khalifa Qadiani hawezi kuonesha orodha ya Muridi japo 20,000 kwa sababu kwa mujibu wa Khawaja Saheb idadi ya jumla ya Ahmadiyya wote Mjini Hindustan haizidi 18,000. Sijui Khawaja Saheb ana hoja zipi zilizompelekea akione kikundi cha Ahmadiaya kama ni cha watu laki 4-5 wakati ambapo hawazidi 18,000. Hiyo ndio kusema, hapana shaka dai la Mian Saheb kwamba yeye ndiye Imam wa watu laki nne mpaka tano(400,000-5000,000) halina msingi wowote.(Akhbar Paigham Sulh, Lahore uk. 5 N 59 ya tarehe 6 Februari 1918).

 

“Lakini wakati hesabu ya watu ikifanywa na serikali ya Uingereza mnamo mwaka 1911 na mwaka 1931, fumbo lote la kukua kwa uhamadiyya  liliporomoka na uongo wa Mirza Ghulam A. Qadiani na waliomfutia ukadhihirika na kuwatia aibu. Idadi halisi ya  watu waliokuwa wakiufuata ukadiani mjini Punjab ambako ndiko ngome kuu ya itikadi hiyo, haukuzidi 55,908.(Mnamo mwaka 1921 idadi ya watu ilikuwa 28,816).( Sensa ya Punjab, Part 1-Ropoti, uk. 313, na Khan Ahmad Hassan Khan, M.A.A., K.S, Msimamizi wa sensa, Pumnjab na Delhi).

Ndugu Msomaji

Imekudhihirika ni namna gani Jamaa wa Makadiani wamekuwa wakiwadanganya watu, akiwemo Mirza mwenyewe, wafuasi wao na magazeti yao. Mirza tahir, Mubashir(Khalifa) wa nne baada ya Mirza naye kadhalika yumo katika hao wanaoendelea kuwadanganya watu hivi sasa. Kwa maneno yake anasema:

“Katika kipindi cha miaka 16 ya Ukhalifa wangu kumekuwa na wimbi kubwa la watu kuingia katika Ukadiani na neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mwaka mmoja tu Uahmadiya ulifanikiwa kupata wageni 3,000,000 hii neem ambayo hata Mataifa makubwa hayangeweza kuiota”.(haya ni matamshi aliyoyatoa Mirza Tahir tarehe 10 juni 1998, na kukaririwa katika Alfazl International, tarehe 26 juni-Julai 2 1998. Uk.4).

“Kwa wakati huu, Jamaat (Ahmadiya) imejaaliwa na Mwenyezi Mungu kuongezeka na kufikia idadi ya wafuasi milioni 10,000,000 na siku zijazo inatazamiwa kuongezeka zaidi kwa kuwa katika kila mwaka makumi ya milioni huingia Jamaat”.

Kama ambavyo Mirza Ghulam alivyowadanganya wafuasi wake kuhusian na kukua kwa Uahmadiya, ndivyo walivyofanya waliomfuatia na Khalifa wa sasa, Mirza Tahir amekuwa akiwadanga wafuasi wake kuhusiana na kukua kwa itikadi yao.

 

Tunatumai kwa ukumbusho huu mdogo Makdiani watajaribu kuuona ukweli. Mirza Tahir hvi sasa akionekana mwenye kukata tamaa amekuwa akijitahidi kuwatia moyo wafuasi wake kwa upande mmoja na kwa upande wa pili na anajaribu kuwashawishi wafadhili wake wa nchi za magharibi kwamba misaada yao inaendele kuzaa matunda na kwamba uahmadiya utashika mahala pa Uislamu kwa kuwa ni itikadi inayokuwa kwa haraka. Ni kwa watu wapuuzi  na mataahira wanaoweza kuamini propaganda hizo. Ukweli unajieleza wenyewe. Amkeni kabla hamjachelewa:

“Haqeeqat Chup Naheen sakte banawat kay usoolon say(Ukweli hauwezi kufichwa na uongo) Khushboo a naheen saktee kaaghaz ka phoolon say ( na harufu nzuri haiwezi kutokana na uwaridi bandia).

 

Wassalaam alaa manittaba’al Hoodaa(amani iwe juu ya wale wanaofuata uongofu).

 

Dr. Syed Rashid Ali

Box 11560

Dibba alfujaira

United Arabs Emirates

http:/alhafeez.org/rashid

rasyed@emirates.net.ae

 

اضيف بواسطة :   admin       رتبته (   الادارة )
التقييم: 0 /5 ( 0 صوت )

تاريخ الاضافة: 26-11-2009

الزوار: 2106


المقالات المتشابهة
المقال السابقة
Al-Zawaid
المقالات المتشابهة
Ahmadiyya Movements - Facts & Fiction
المقال التالية
Open Letter to Mirza Masroor
جديد قسم مـقـالات الموقـــع
القائمة الرئيسية
البحث
البحث في
القائمة البريدية

اشتراك

الغاء الاشتراك