n> 158). Shairi lifuatalo lilisomwa mbele ya Mirza ambaye alilipenda na aliripotiwa kusema Jazakallah shairi hilo lilikuwa na sehemu ambayo ilibandikwa ukutani isemayo:
"Muhammad ametumwa tena miongoni mwetu na atakayekuwa mkubwa zaidi kuliko kabla ya hapo. Aanayetaka kumuona Muhammad katika ukamilifu anapaswa kumuangalia Ghulam Ahmad wa Qadian"
(Shairi hilo lilitungwa na Qazi Zahoor Ahmad Akmal Qadian ambalo lilisomwa mbele ya Mirza Qadian, lilichapishwa katika Gazeti la Paigham us Sulh la tarehe 14 Machi, 1916)
Kwa mwanga wa maandiko hayo hapo juu, Machapicho rasmi ya Makadiani yalieneza imani imani hii:
"Hivyo yupo yeyote mwenye shaka kwamba Mwenyezi Mungu amemtuma Muhammad(s.a.w) tena katika nchi ya Kadiani kukamilisha ahadi yake?(Kalimat al Fasl na Mirza Basheer Ahmad mtoto wa Mirza Ghulam A. Qadian, Review of Religions uk. 105, Na. 3. juzuu 14).
Taji la Masihi aliyeahidiwa , mbele ya Mwenyezi Mungu ndilo Taji la Mtume(s.a.w). Kwa maneno mengine, katika kumbukumbu za Mwenyezi Mungu hapana uwili au tofauti kati ya Masihi aliyeahidiwa na Mtume(s.a.w). Wote hao wawili wana hadhi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu. Kwa nafasi, hadhi na jina hilo. Ingawa kimaneno wao ni wawili lakini kiuhalisi ni mmoja na ni huo huyo."(Alfazl, Qadian, juzuu 3, No 37 tarehe 16 Septemba 1915, kama ilivyoandikwa ka Qadian Mazhab uk 207, chapisho la 9, Lahore).
Masihi Mowood si kitu kingine kinachotofautiana na Mtume(s.a.w), lakini ni yeye ambaye amekuja tena katika ulimwengu akiwa katika sura halisi...Kwa hiyo kuna shaka yoyote kwamba Mwenyezi Mungu amemtuma tena katika Qadian?"(Kalimat Alfas uk.104-105, Review of Religion Qadian March 1915.
Hitimisho
Ni wazi kutokana na kile kilichosemwa hapo juu kwamba ndio dini ya Ukadiani kuwa imani zifuatazo:
. Mirza ni Mtume na mjumbe wa Mwenyezi Mungu
. Mirza ni Muhammd aliyekuja kwa umbo lingine
. Mirza hatenganishwi na Mtume(s.a.w)
. Mirza ana hadfhi sawa na Mtume(s.a.w)
. MIrza ni mbora kuliko Mtume(s.a.w)
. Mirza ni mtume wa mwisho
. Kwa hiyo Mirza ndiye Khatam un Nabiyin
Tahadhari:
Pale Qadian anapodai kuwa anamini Mtume(s.a.w) kama Khataman Nabiyyin au akitamka Kalima Tayyiba, ambayo sisi Waislamu tunaitamka, ni wazi anakudanganya. Ni kweli anatamka maneno yale yale lakini akimjumuisha na Mirza katika maan yake. Ni kweli anasema Muhammad ni Khataman Nabiyyin lakini akiwa na maana tofauti. Anamaanisha MIrza ni Muhammad aliyekuja katika umbile jingine, kwa Qadian Mirza ni mtume wa mwisho na kwa hiyo ndiye huyo Khaataman Nabiyyin.
Kwa mujibu wa Fatwa yake, iliyotajwa huko nyuma Mirza ni mdanganyifu, mzushi,, si muumini wa Qur'an, anaipinga Qur'an, muongo, Murtad, sio Muislamu, adui wa Qur an ana hana haya mbele ya Mwenyezi Mungu.
Yaa Allah waepusha waislamu na imani ya Ukadiani iliyojighushia jina la Uislamu. Ya Allah warejeshe kwenye njia sahihi wale waliopotea kwa bahati mbaya kutokana na udanganyifu wa Ahmadiyya?
Wassalaam alaykum alaa mani tTaba'al hudaa
Amani iwe juu ya wale wanaofuata uongofu.
Dr Syed Rashid Ali
P O Box 11560
Dibba Fujairah
United Arab Emirates
rasyed@emirates.net.ae
http://alhafeez.org/rashid/