" dir="ltr" class="MsoBodyTextFirstIndent2">Mirza anakaririwa kusema: “Kitu ambacho hakina mfano wa kukilinganisha nacho, hii kwa maneno mengine inaitwa Khaariq-i-Aaadat.” (Roohani Khazain vol. 22 uk. 19) ”Khaariq-i-Aaadat” inaelezwa kuwa ni kitu kisicho na mfano katika ulimwengu.” (Haqiiqatu Wahi. Roohani Khazain vol. 22 uk. 19) Kwa kweli kilichotokeya ni kwamba mtu ambaye kinafiki alijifanya muumini aliingiya katika kundi la wanafunzi wa Lekhram, na alikuwa akiviziya kupata nafasi nzuri na punde tu alipomuona Lekhram yuko peke yake, alimtumbuwa na kumuuwa na yeye akatoweka.
Maelezo yafuwatayo yanatoka katika jarida la Ahmadiya kutoka Karachi,
‘Souvenir’:
Jumamosi, machi 6 1897 inaelezewa hivi kwamba Pandit Lekhram alikuwa nusu uchi akifanya Sindhiya (ibada ya kidini) ghorofani. Baada ya kumaliza Sindhiya alijinyoosha ambapo tumbo lake likachomoza kwa mbele. Muislamu aliyenyowa kichwa na kuwa Muhindu alikuwa amekaa karibu akiwa amejigubika blanketi. Akalitufuwa tumbo la Lekhram kiyasi kwamba utumbo wote ukatoka nje”. (Souvenir uk. 70)
Mirza Ghulam ana haya ya kusema kuhusiyana na tukiyo hilo:
”Katika hili jambo la Lekhram kazi ya mkono usioonekana inaonekana wazi kabisa. Kajiwa na mtu aliyenyowa ,akamwamini sana mtu huyu kiyasi kwamba akamchukuwa nyumbani mwake bure tu. Jioni kuondoka tu wageni wengine, wakabaki wao tu wawili, kwa kweli siku ya pili ya Eid akafanya kazi aliyoiendeya, kuinuka tu Lekhram kutoka katika kazi ya kuandika na kujinyoosha huku akilipeleka tumbo mbele na pigo la jambiya likaleta maafa na hadi wakati wa kifo chake, Mungu kafunga mdomo wake kiyasi kwamba licha ya kuwa na fahamu zote na kujuwa kuwa mimi nimetabiri dhidi yake hakuelezeya tuhuma zake hata kidogo kuwa namtuhumu Mirza Sahiib; na mpaka leo hii muuwaji hajaonekana- Yote hii ni kazi ya Mungu ambayo inaogopesha, ikionesha mamlaka na uweza wake” (Roohani Khazain, Malfuuzat of Mirza Ghulam Ahmad Qadiani vol. 10 uk. 170-171). Wasomaji msome kwa makini nukuu ya hapo juu. Taswira ya mazingira ya dakika za mwisho za Lekhram ambayo Mirza ameichora, ingawaje ni ya kutowa lawama, inazusha swali moja muhimu. JE MIRZA GHULAM ALIIJUWAJE HABARI HII? MIRZA ALIJUWAJE KUWA LEKHRAM ALIINUKA GHAFLA KUTOKA KATIKA KAZI YA KUANDIKA, AKAJINYOOSHA KWA NAMNA AMBAYO TUMBO LAKE LILITOKEZA MBELE NA PAPO HAPO MUUWAJI AKAMTUMBUWA NA JAMBIYA?
Kuna watu wawili tu ambao waliijuwa habari hii. Yule aliyeuwa na yule aliyeuliwa. Naam, Allah piya Anajuwa lakini hakuna sehemu yoyote katika vitabu vyake ambapo Mirza amesema kuwa Mungu alimfahamisha habari hii.
Lekhram hakuwapo tena duniyani kuweza kusimuliya tukio hilo. Mtu pekee ambaye angeweza kumpa habari ya tukio hilo Mirza ni yule aliyefanya mauwaji hayo (muuwaji).
Kwa maneno mengine, maelezo haya ya Mirza Ghulam yanafichuwa uhusiyano wake na muuwaji huyo. Je kuna Ahmadiya/Kadiyani yeyote anayeweza kutuambiya Mirza Ghulam alikuwa na uhusiyano wa aina gani na muuwaji huyo kiyasi kwamba aliweza kumpatiya maelezo haya ya mtu aliyeshuhudiya tukiyo kwa macho yake? Na kwa nini Mirza hakumkabidhi muuwaji mikononi mwa Polisi/kama kweli muuwaji hakuwa mmoja wa wafuwasi wa Mirza Ghulam, basi je haiwezekani kuwa alikuwa muuwaji aliyekodiwa? Kuhusiyana na hili, maelezo haya mengine ya Mirza Ghulam yana jambo muhimu:
“Utabiri wa nabii wa uwongo (mzushi) kamwe hautimii. Mungu husimama dhidi yake ili ulimwengu usiangamiye, kama vile Lekhram kwa kuudanganya ulimwengu,alitowa tangazo juu yangu kuwa nitakufa ndani ya miyaka mitatu. Mbona hakuweza kula njama na muuwaji ili utabiri wake utimiye?” (Roohani Khazain vol. 12 uk. 25) Nukuu hii inaonesha kuwa Mirza Ghulam alikuwa anajuwa jinsi ya kushirikiyana na muuwaji kumuuwa mtu!!
Jarida la Ahmadiya ‘Souvenir’ linaandika hivi:
“Watu wanasema kuwa walisema (mke na mamaake Lekhram) kuwa walimuwona muuwaji akishuka ghorofani” (Souvenir uk. 70)
Mirza Bashir Ahmad, mtoto wa Mirza Ghulam kaandika hivi:
“Kauli ya mke wa Lekhram ilisikika, mtu aliyemuuwa Lekhrama baada ya kuuwa akapanda ghorofani na kwenda kwenye paa.” (Tabligh-i-Hidayat uk. 188).
Swali ni hili: Kama Lekhram aliuliwa na malaika kama mubalighi wa Ahmadiya wanavyotaka tuamini, alikuwa na haja gani basi ya kuingiya katika kundi la waumini na kuviziya apate fursa ya kumuuwa Lekhram na kisha baada ya kumuuwa ashuke au kupanda ghorofani? Si angeliweza kutokeya na kutoweka mle mle ndani bila kuonwa na mtu yeyote. Au Malaika bila kuonekana angeweza tu kuuwa mbele ya waumini-hiyo ndiyo ingekuwa ajabu.
Huu ni ushahidi wa kimazingira ambao piya uliifanya Polisi isadiki kuwa kulikuwa na njama ambapo Mirza Ghulam piya alihusika . Mara mbili Polisi walivamiya nyumba yake lakini Mirza Ghulam naye hakuwa mwanafunzi katika jambo hilo:
“Watu hawa walijuwa fika katika nyoyo zao kuwa hii ilikuwa kazi ya Mungu na si mpango wa mtu aliyetowa utabiri, lakini bado kwa maombi ya mara kwa mara ya serikali kupekuwa nyumba yangu na kwa kuleta heka heka nyingi wakatekeleza mapatano yao na watu wanaoabudiya ng’ombe.” (Roohani Khazain vol. 12 uk. 54)
“Mnamo Aprili 8, 1897 nyumba yangu ilipekuliwa” (Roohani Khazain vol. 12 Uk. 55).
Muuwaji katu hakukamatwa, serikali ya Uingereza haikufanya chohote zaidi ya kupekuwa nyumba licha ya kelele nyingi za shutuma kutoka kwa wahindu. Ni wazi walilazimika kumkinga pandikizi wao kwa mpango mkubwa zaidi.
Kisingiziyo kingine cha kushindwa kufanya muujiza “Ni kwa sifa gani mtu Muwongo anayekula mizoga eti Mbingu imuoneshe ishara na ardhi imuoneshe maajabu yasiyo ya kawaida?” (Roohani Khazain vol. 12 uk. 3)
Mirza Ghulam akaandika maneno ya kujihukumu mwenyewe “Tunamuona huyo Kiongozi wa Kiroho na piya Hao wanafunzi ni mbwa kabisa na mfumo wa maisha yao ni wa kishenzi kabisa ambao wanatowa tabiri majumbani na kisha kwa mikono yao wenyewe, kwa ujanja ujanja na kwa ghiliba wanajaribu kuzitimiza wenyewe na kuwalazimisha wengine wazitimize. (Roozani Khazain vol. 12 uk. 27)
Mwaliko kwa Khalifa mteule wa Jumuiya ya Ahmadiya, Mirza Masruur Ahmad Tunamwalika Khalifa mpya mteule wa tano, Mirza Masruur Ahmad Qadiani kuwa ama ajitokeze na kufanya nasi Mubahila juu ya suwala la Lekhram au vinginevyo atangaze kwa kiyapo (kwa sharti la kupata adhabu ya Mungu ikiwa anakula kiyapo cha uwongo) kwamba Mirza Ghulam Ahmad hakuhusika na mauwaji ya Lekhram, kwamba mauwaji ya Lekhran hayakufanywa kwa mikono ya kibinadamu bali malaika na mwisho ni kuwa utabiri wa Mirza ulitimiya.
Ziyara ya Ahmadiya wa zamani, Ahteshamul Haq Abdul Bari nchini Ubelgiji
Kiongozi wa harakati dhidi ya Ahmadiya/Ukadiyani mjini Mumbai, India alifanya ziyara nchini Ubelgiji mnamo mwezi Desemba mwaka 2003. Wakati wa ziyara yake alikutana na mtu aliyerejeya katika Uislamu ambaye alinaswa na mtego wa Ahmadiya.
AlHamdulillah pale Sheikh Ahtesham alipomuelezeya undani halisi wa Ahmadiya, mtu huyo akaikana Jumuiya hiyo. Baada ya hapo akamuwalika kwenye Kituo cha Ahmadiya mjini Antwerp ili wawe na majadiliyano na mubaligha wa eneo hilo.
Murabi wa eneo hilo, Nasir Ahmad Sindhi akaitisha mhadhara wa kuzungumziya faida za swaumu uliofanywa kwa lugha ya Kiingereza. Wakati wa hotuba yake aliielezeya Jumuiya yake kuwa ni Jumuiya inayopenda amani na kuwaelezeya Waislamu wengine kuwa ni wanamgambo. Alipomaliza hotuba yake, mbele ya hadhara Ahtesham akajaribu kuuliza maswali fulani kuhusu Mirza Ghulam Ahmad Qadiani, mwasisi wa Jumuiya ya Ahmadiya lakini akazuiliwa. Hata hivyo baadae akafanikiwa kuzungumza na Ahmadiya waliokusanyika hapo juu ya madai ya Mirza Ghulam. Murabi Nasir Sindhi alizungumza kwa niyaba ya Ahmadiya. Miongoni mwa waliokuwepo ni Bw. Hashmi, Malik Naiim, Khaliq Iqbal, Hafiiz Butt Saheb, Chaudhary Mansuur Ahmad Sialkoti na wengineo. Mbele ya watu hao, pakafanyika Mubahila kati ya Ahtesham na Ahmadiya juu ya ukweli na uwongo na wakaomba laana ya Allah iwashukiye waongo kwa kusema Laanatullah ‘ala-al kadhibiin.
Bw. Ahtesham piya alimuwomba Bw. Murabi ampatiya seti nzima ya vitabu vya Mirza Ghulam Ahmad kwa bei yoyote ile. Kwanza Murabi Saheb aliahidi kuwa angempatiya vitabu hivyo lakini baadaye akaghairi. Wakati wa mdahalo Murabbi Sahib na Chaundhry Mansuur Ahmad walipata hasira na kuanza kumuapiza yule mtu aliyerudi katika Uislamu na kutishiya kumpiga. Sheikh Ahtesham akawakumbusha kuwa vurugu siyo njiya ya mahubiri katika Uislamu na akawaambiya kuwa kama wakienda kwenye misikiti ya Waislamu watakuta mwenendo tofauti kabisa.
Tunamuwomba Allah awape tamiizi wafuwasi hawa waliopoteya wa
Ahmadiya waweze kupambanuwa haki na batili na awape hidaya wafuwate
njiya sahihi. Amiin
Wa maa alainaa ila-albalaagh
Wassalaam ala mun-ittaba’a al-huda
Dkt Syed Rashid Ali