AlFatwa 8

Bismillahir Rahmaanir Rahiim

Harakati za Wapinzani wa Ahamadiyya katika Uislam

Kwa jina la Allah Mwingi wa Rehema Mwenyekurehemu Mapenzi na Amani ya Allah imwendee Syidna Muhammad na familia yake na wafuasi wake

 

AlFatwa ya Kimataifa ya 8

Kwa nini Niliukana Uahmadiyya? Na Dr. Ismail. A. B. Balogun

Aliyekuwa mfuasi wa Ahmadiyya wa cheo cha juu.

Ni lazima niseme, mbele ya Mungu na Watu jinsi nilivyochambua zaidi madai na kumbukumbu za kwao, niligundua zaidi kuwa Jumuia ya Ahmadiyyah ni ya kudanganya ulimwengu na kuchezea ujinga wa wafuasi wao wengi. Dr. Balogun.

Katika mfululizo wa makala yaliyochapishwa Nigeria katika mwaka 1974, Dr. Ismail A. B. Balogun, mfuasi wa Ahmadiyyah wa cheo cha juu, alikanusha mafundisho ya Ahmadiya na alikana hadharani Jumuia aliyozaliwa ndani yake na kulelewa. Profesa wa masomo ya Kiislamu na Lugha ya Kiarabu katika Chuo Kikuu cha Ibadan, Nigeria, Dr. Balogun aliyatoa mhanga maisha yake kutetea Uahmadiyah na aliweza kupanda daraja hadi kufikia kuwa msemaji wa cheo cha juu wa Jumuia yake kwa miaka mingi, mahubiri na mihadhara yake ya kimahiri na ya jazba kujitoa kwake dhahiri shahiri (kutoka jumuia ya Ahmadiyah) kulizusha vurugu na majadiliano makali yaliyozindua watu wengi wasomi kuutambua ukweli na kuachana na Ahmadiyah.

Toba inayopokelewa na Allah (SWT) ni ya wale wanaofanya uovu kwa ujinga, kisha wakatubia kwa upesi. Hao ndio Allah (SWT) huipokea toba yao. Na Allah (SWT) ni Mjuzi na Mwenye hekima. (Quran An-Nisaa, 4:17)

Kisha ndipo Dr. Balogun alipotayarisha maandishi yenye kuelezea sababu zake za kujitoa kutoka jumuia na kuweka majadiliano yaliyojiri katika kitabu chake alichokiita: “Islam dhidi ya Ahmadiyah katika Nigeria”. Katika kitabu hiki Dr. Balogun alifichua siri jinsi yeye, sawa na watu wengine wengi wasomi walivyokubali uaAhmadiyah kutokana na kuwaheshimu wazazi wake, upotoshaji wa mafunzo ya viongozi wa Ahmadiyah na uzandiki wa mbinu za Wamisionari wa Ahmadiyah wa Kipakistani, na akatoa sababu wazi zinazoelezea mapenzi ya kimadhehebu zaidi kuliko ukweli wa Ahmadiyah.

Dr. Balogun anaelezea makuzi yake na imani yake ya kibubusa kwa wamisionari wa Ahmadiyah wa Kipakistani katika kitabu chake kama ifuatavyo:

"Katika utoto wangu nilikuzwa kuwathamini sana Wamisionari wa Kiahmadiyya Wahidni na Wapakistani ambao walilinda na kuongoza shughuli zetu za kidini. Ujumbe ulipofika kwa wazee wetu na kwa kupitia kwao kuja kwetu, tuliamini yote waliotueleza kwa jumla kwa sababu ya imani yetu ya dhati kwao.

Mahubiri yao yalikuwa na maana kwetu, na tulizikubali hoja zao katika nia njema. Walichukua marejeo kwenye Vitabu vya Kiislam ili kuzipa uzito hoja za madai yao na tulikubali nukulu hizo bila kuzitilia shaka wala bila kuzichunguza kwa sababu ya Imani tuliyokuwa nayo kwao.

Utaratibu wao ulikuwa na nia ya kututenga dhidi ya Imani ya Ukweli ya Kiislam ambayo waliitia dosari katika hali yao ya kufanya Ibada za Kiislam. Wamisionari walidai kuleta “Uislam wa kweli” kwetu sisi kwa jina la Ahmadiyya.

Mara nyingi walitufanya tuamini kuwa upinzani mkali walioupata Waahmadiya huko India kabla ya utengano na baadaye katika Pakistani, ulikuwa ni ushahidi tosha wa ukweli wa Ahmadiyyah. Tangiapo, hakuwa Nabii anayekubalika moja kwa moja katika mji wake au nchi yake. Hoja hii ilituridhisha sana hivyo tuliwafuata bila ya wasiwasi na kwa imani thabiti.

[Islam dhidi ya Ahmadiyah katika Nigeria, uk. 85 – 86]

Zaidi ya robo ya karne iliypoita, Dr. Balogun alifafanua kwa uhakika mbinu zilizotumwia na Wamisheni sio tu kwamba hawahubiri kwa uwazi picha kamili ya mafunzo na historia yao, lakini pia kwa nguvu sana walivuruga na kupotosha mafunzo ya Uislam na yale ya Wasomi wa Kiislam na kujaribu kuweka mambo yanayoharibu kwa kuyakuza kwa kuwatumia Waislam wasiokuwa na elimu Dr. Balogun alinakili:-

“Japokuwa Uahmadiyya umekuwepo kwenye nchi hii karibu miaka sitini, natoa uamuzi kwa Imani kuwa mpaka sasa watu wengi kabisa wenye mshikamano mkubwa mno katika jumuiya na misheni yao bado wako gizani kuhusu undani wa mafundisho pamoja na umuhimu wake. Kwa mfano ni hivi karibuni tu upinzani mkali wa Waahmadiyya umejitokeza kichwa juu katika nchi hii kwamba kwa mara ya kwanza viongozi wa ngazi za juu za uongozi walielewa kuwa Mirza Ghulam Ahmad alidai kuwa yeye ni “Mtume” (Ibid. Ukurasa wa 3).

[Ukweli kwamba Waahmadiyya walificha ukweli wa mafundisho ya dini kwa wanachama wao walio wengi ni] “Ushahidi wa ukweli kwamba kijana msomi wa Kiislam katika Nigeria ambaye mwanzo alijiingiza ndani ya jumuia hapa, baada ya kwenda Uingereza kwa masomo ya juu na kukutana na Ahmadiyya wa Kihindi waliokuwa wakiishi Uingereza, akajifunza kutoka kwao kwa karibu zaidi na aliporudi nyumbani aliachana na jumuia hii. Huyi alikuwa hayati al-Haj L.B. Ahusto wa kumbukumbu zilizobarikiwa (Ibid ukurasa wa 2).

Kwa uhakika, tokea mwanzo viongozi wa Ahmadiyya walitumia njia za Wamisionari wa Kikristo zilizohakikiwa kufarakanisha wenye ujuzi na wasiokuwa na ujuzi ili kuongeza idadi ya wanachama wao. Walielewa wazi kwa vizazi vya waumini waliozugwa na kujiunga na jumuiya yao watakuwa si rahisi kuachana na jumuia hata kama wakielewa ukweli.

Ni kweli waliwafuata baba zao kwenye njia mbaya; kwa hiyo na wao pia walianguka chini kwenye nyayo zao! Na kabla yao, wengi wa wale wa kale walikuwa kwenye njia ya upotofu. (Qurran Takatifu, As-Saafat, 37:69-71)

Dr. Balogun aliweka kumbukumbu kwamba katika mwaka 1974 kuwa serikali ya Pakistani na Jumuiya ya Kiislam ya Ulimwengu walitangaza kwua Ahmadiyya si kundi la Uislam, aliweka mikakati ya kutetea ukweli wa jumuiya ya Ahmadiyyah aliozaliwa. Hata hivyo utafiti wake wa kina na kisomi wa mafunzo ya uongozi wa Ahmadiyyah ulimwondolea utanod wa giza na haukumwachia chochote bali kujitoa kutoka jumuiya ya Ahmadiyyah. Matokeo haya ni muhimu sana kwani Dr. Balogun pamoja na kuwa yeye ni kiongozi wa ngazi ya juu ya jumuiya ya Ahmadiyyah, alikuwa gizani kuhusu ukweli wa Ahmadiyyah kwa miaka arobaini kuhusu nukulu za visingizio zinazotolewa na wamisionari wa Kiahmadiyyah kutoka kwenye Quran, Hadith na maandiko ya wanazuoni wa Kiislam kuunga mkono madai yao; Dr. Balogun anaandika:-

“Madhamuni yangu (katika kuthibitisha tena marejeo yanayotolewa na Ahmadiyyah) ilikuwa ni kujiimarisha dhidi ya upinzani mkali kwa Ahmadiyyah. Nikiwa msomi wa Chuo Kikuu nilikuwa na mwamko kwamba matamshi yangu katika kuunga mkono Uahmadiyya lazima yawe na uhakika wenye marejeo na hoja halisi za vyanzo asili vya Kiislam.

Katika kuthibitisha marejeo ya wamisionari wa Kiahmadiyyah, hata hivyo ugunduzi wangu ulikuwa  si wa kuridhisha. Ni lazima niseme mbele ya Mungu na mwanadamu, kwamba jinsi nilivyochunguza zaidi nukulu za madai na taarifa juu yao, ndivyo nilivyogundua zaidi kuwa ujumbe wa Kiahmadiyyah ulikuwa wa kudanganya ulimwengu na kuutumia ujinga wa wafuasi wake wengi.

Mara nyingi hunukuu watunzi (wasomi) ambao wako wazi kupinga mawazo ya Ahmadiyyah; lakini kwa akili sana huandika nukulu hizo kutoa mwelekeo wa kuona kuwa watunzi wanaunga mkono mwelekeo wa ahmadiyyah. Namna pekee ni kwenda kwenye vyanzo vya mwanzo na kusoma yale yaliyo dondolewa na Ahmadiyyah kwenye muktadha wa maandishi yalivyowekwa ili msomaji, na mtafiti wa ukweli, ataona kiasi gani Wamisheni wa Ahmadiyya wa Pakistani walivyojaribu kudanganya Ulimwengu” (Ibid ukurasa 86-87).

Katika uchunguzi wa ndani wa Dr. Balogun juu ya vyanzo vya asili na uhalisi wa vitabu vya Kiislam umeweka wazi kuwa Waanzilishi na Viongozi wa Kiahmadiyyah walichangamkia na kwa makusudi waliamua kudanganya na kupotosha wasiojua. Ndani ya kitabu hiki amefafanua ugunduzi huu:

“Ni wazi ktuokana na nukulu ambazo jumuia imezidondoa walizodhani zingewasaidia kuunga mkono mtazamo wao wa makosa kwa sherehe ambayo ni kinyume na msimamo wao. Hii ni, ili kutoa fikra kuwa mtunzi anaunga mkono mawazo yao. Katika jamii za kielemu kitendo hiki cha kuharibu mtazamo wa mtunzi na fikra inakwenda kinyume kanuni ya Kimataifa ya kunakili makala. Ni kweli, haikubaliki na haiwi ni mtazamo pia, ni kitendo cha kuchukiza. Fikiria kwa mfano, Qurran ambayo husema, “kuvunja sheria hubadili taratibu kutokana na vile zilivyotengenezwa; kwa hiyo tunatuma, madhara kutoka peponi kuja kwa wavunjaji wa sheria kwa kufanya upotofu”. “Chakula cha fikra hakika ni kwa ajili ya Ahmadiyya”. (Ibid ukurasa wa 94-95)

Ni kwa wale ambao hawaziamini alama za Allah hughushi mambo kwa kukumbatia uongo: Ndio ambao hudanganya! (Quran Takatifu, An-Nahi, 16:105)

Kufuatia tangazo lake la dhahiri, Dr. Balogun amekuwa mshutumiwa mashambulizi ya kutoka kwa Wamisheni wa Kiahmadiyyah wa Kipakistani. Mathalani, Molvi Ajmal Shahid, baadaye alikuwa Amir wa Jumuiya ya Ahmadiyyah wa Nigeria alitoa jibu fupi mno ambamo onyesho la “kifo cha Kiimani kaka, (Ibid ukurasa 97)’ na Moulvi Naseem Saifi; Mkuu wa Misheni ya Ahmadiyyah wa Afrika ya Magharibi , alithibitisha kuwa Dr. Balogun alijitenga na Ahmadiyyah kwa ajii ya kuupa nguvu Uislam (Ibid ukurasa wa 99); bado Wamisheni wengine wa Kiahmadiyya waliendelea kumuuliza maswali juu ya nia yake kwa umma kutokana na kujitoa kwake katika jumuia.

Katika kuweka wazi mambo, Dr. Balogun ambaye kwa muda wa miaka mingi ametambua na kuelewa mbinu za viongozi wa Ahmadiyyah kwa kuwaaibisha wale wanaoukana Uahmadiyyah.

“Ningeweza kutoa nukta zote kwenye makala hii juu yao (viongozi wa Ahmadiyyah wa Kipakistani) kwa udnani bila matangazo yoyote yale ya hadharani; lakini uzoefu umenionyesha kuwa ukosoaji huo moja kwa moja utaleta muda mrefu wa kutengwa kabisa na jamii. Kutokana na haya yote, hakuna hata mwanachama mmoja ambaye angekuwa tayari kunisikiliza. Nilikwihsa toa maelezo ya msimamo wangu, Mungu ndiye shahidi, haswa ni kwa sababu ya umakini wangu juu ya uwajibikaji ulionibidi juu ya jamaa zangu Wanigeria hasa Waislam, na Waislam wa Ulimwengu mzima kwa jumla. Lengo langu halikuwa kuwapinga Ahmadiyyah; niliishi ndani yake kwa muda wa kutosha kuweza kulainisha moyo wangu. Lakini pamoja na hali hiyo kila upinzani wa mawazo ulijitokeza kati ya Uislam na Ahmadiyya itanibidi kuukubali Uislam bila maneno ya kificho” (Ibid ukurasa wa 17).

Tuna imani kuwa watu binafsi waliojiunga na Ahmadiyyah watafikiria upya msimamo wao ilivyokuwa mwanga wa ushahidi umetolewa na Dr. Balogun. Jee itakuwa kwa wale wote ambao wameguswa na mujiza wa Quran na mafundisho ya Mtume wa mwisho, Muhammad (S.A.AW) wanaweza kuthibitisha uaminifu kwa Allah (SWT) na mtume wake wa mwisho (S.A.A.W) au kwa wale ambao wenye mwenendo wa udanganyifu

unaoendelea kutolewa.

Kwa hakika wale waliokufuru Allah, na kawazuilia (watu njia ya Allah na Mtume baada ya kuwabainikia uwongofu wao, hawamdhuru Allah hata kidogo ila ataviondoshea thawabu vitendo vyao visiwe na ataviangusha (Quran Takatifu, Muhammad 47:32).

Madondoo yamechukuliwa kwenye: Islam dhidi ya Ahmadiyyah katika Nigeria. Zimechapishwa na Sh. Muhammad Ashrat, Kashmiri Bazar, Lahore, Pakistan.

Kwa hisani: Anti Ahmadiyya Movement in Islam P O Box 11560, Dibba, Al-Fujairah U.A.E. http://alhafeez.org/rashid/

Idara Dawat-u-Irshad, USA Inc. P.O. Box 22885, Alexandria VA 22304 http://www.irshad.org/idara/

Wanaharakati wapinzani wa Uhamadiyyah katika Uislam

Dr. Syed Rashid Ali P.O. Box 11560 Dibba al-Fujairah Jamhuri ya Falme za Kiarabu

http://alhafeez.org/rashid/

تاريخ الاضافة: 26-11-2009
طباعة