Religious Adventurism

Anti ahmadiyya Mouvement in Islam

Umbambala wa Kidini katika Uislamu

Tahira Parwez

Waislamu wanamuamini na kumfuata Muhammad (saw) kama Mtume wa mwisho, na wanaamini Qur’an kama Kitabu kitukufu cha Allah. Kugeuza au kupotosha imani hii kwamtoa mtu nje ya wigo wa Uislamu. Uislamu, kama zilivyo dini nyingine, umekumbwa na umbambala wa kidini kwa sura ya wazushi wa unabii tangu kuanza kwake. Wengi kati ya wazushi hawa, dhahiri shahiri, walikuwa punguwani na walipuuzwa au walitibiwa ipasavyo, wengine walikuwa ni wajanja waliokuwa na tamaa za kisiasa. Hawa wa kundi hili la pili, waliohesabiwa na Allama Iqbal kama wambambala wa kidini, ndio mada ya makala hii. Kuwepo kwao, kwa kiasi kikubwa, kwatotakana na kuibuka kwa Uongozi wa Kimula chini ya Uislamu wa kibeberu na kutanuka kwake hadi kuwa utumishi wa kitaasisi hasahasa pale dola ya Kiislamu ilipokuwa inasambaratika.  Musaylima, Sajdah, al-Aswad al Ansi, na Tulayha b. Khuwaylid walidai unabii wakati wa Muhammad (saw) na muda mfupi baada ya kutawafu kwa Muhammad (saw). Hawa wanafahamika kama viongozi wa ridda waliokataa kutambua mamlaka ya Dola ya Madina ili kukidhi matakwa yao ya kupata uhuru wa kikabila na kieneo. Al-Aswad, ‘mtu aliyefichikana,’ ndiye aliyekuwa kiongozi wa kwanza wa ridda nchini Yemen. Kuna kuhitilafiana iwapo alikuwa Muislamu. Yeye alidai kuwa ni mtabiri (khain), alinena kwa jina la Allah na akafanya mazingaombwe. Baada ya kumuua kiongozi wa kabila lake, Sahar, akawakata vichwa wajumbe wawili wa Muhammad (saw) na akatangaza uhuru wake. Utawala wake ulidumu kwa miezi miwili tu kwa sababu wafuasi wake na mjane wa Sahar ambaye alimuoa, walimuua.  Musaylima (al-kazab) alijitangaza nabii baada ya kifo cha Howda ili aendeleze dai lake la kuwa kiongozi wa Banu Hanifa (630 AD). Aliamrisha sala tatu, funga, na kukataza pombe ( akapingwa!). Pia aliamini kufufuliwa.  Alipingwa vikali pale alipomuandikia barua Muhammad (saw) mwaka 632 AD kwa ajili ya mgawanyo wa mamlaka. Abu Bakar (r.a) akamtuma Khalid b. Walid (r.a) na jeshi kubwa ambaye alihitimisha maisha yake na matamanio yake. Muda mfupi kabla ya kufa kwake,Musaylima alimuoa Sajdah, mwanamke aliyedai unabii kutoka kabila la Tamim. Al-Harith b.  Said alidai unabii katika kipindi cha Khalifa wa Banu Umaiyya, Abd al-Malik b. Marwan. Askari wengi waaminifu walituhumiwa kumuunga mkono. Huyu akanyongwa mwaka 698-699 AD. Imam Abu Hanifa aliamini barabara mwisho wa unabii, khutum-e-nabuwaat na akafutu kuwa Muislamu huwa kafiri hata tu akimuomba mzushi wa unabii ampe uthibitisho wa dai lake.  Alimpinga na kumkosoa vikali mtu mmoja asiyefahamika jina ambaye alituhumiwa kuwa na nia hiyo katika zama zake (699-767 AD). Muasi mmoja mashuhuri wa Kishia al-Mukhtar b. Abi Ubayd naye pia katuhumiwa kudai yeye ni nabii. Muhammad b. Sa’id (al-Muslub) anasadikiwa kuwa mmoja wa watu wanne waliogushi Hadith. Yeye ndiye aliyepotosha Hadith isemayo, "Mimi ndiye komeo la manabii na hakuna nabii baada yangu." Akaongeza maneno haya, "isipokuwa akitaka Allah". Kwa kutia nyongeza hii, bwana huyo akaripotiwa kudai unabii. Bwana huyu alinyongwa kwa amri ya Khalifa wa Banu Abbas, Abu Jafar al-Mansur. Hashim b. Al-Hakim, aliyejulikana katika historia, kama al-Muqanna, alidai unabii katika mji wa Khurasan wakati wa uongozi wa Khalifa wa Banu Abbas, al-Mahadi.  Akaripotiwa kupata wafuasi fulani katika eneo hilo. Alikamatwa na kunyongwa mwaka 779-780 AD baada ya kushindwa na majeshi ya Khalifa huyo.

Mahmud b. Al-Faraj alijitokeza mjini Samara mwaka 849-850 AD akidai Qur’an ilifunuliwa kwake kupitia Malaika Jibril. Akaripotiwa kupata wafuasi fulani katika miji ya Samara na Baghdad. Alinyongwa kwa amri ya Khalifa, al-Mutawakkil. Mirza Ali Muhammad, aliyejulikana kama mlango (Bab), alizaliwa mwaka (1819 AD) na akakulia mjini Shiraz, nchini Iran. Alipata elimu ya kisasa hadi alipofikisha umri wa miaka 15, baada ya hapo, aliingia katika biashara na mjomba wake. Alioa akiwa na umri wa miaka 22 na akapata mtoto ambaye alikufa angali kichanga. Katika jamii ya Shia, Imam wa Ughaibuni alitazamiwa kutokea mwaka 1260 Hijiria (1844 AD) jambo hilo lilienda sanjari na kumbukumbu ya elfu moja ya kutoweka kwake. Bab alikuwa karibu na dhehebu la Shaykh ambao waliamini kuwa nabii wa Mungu alikuwa mbioni kutokea.

Pale Bab alipojinadi yeye ni Mlango wa kumuelekea Imam wa 12 na kutoa madai mengine, akakumbatiwa na mashaykh, sasa wakaitwa Babis (wafuasi wa Bab). Baadae Bab akajitangaza kuwa yeye ni Imam wa Ughaibuni, akiendeleza dai la dhehebu la mashaykh kuwa Imam huyo wa Ughaibuni anaishi kwa taswira zenye sifa zote muhimu (Hurqalya), kwa hiyo kurejea kwake sio katika umbile lilelile la mwili bali ndani ya mtu ambaye ni mfano halisi wa Imam huyo. Baada ya Mahd (Imam aliyefichikana), aliendelea kujiita Nuqtiyiula (sifa ya Muhammad (saw) na akatangaza kuwa Qur’an na Sharia ya Kiislamu sasa zilitanguliwa. Wanazuoni wa Shia na Sunni walimlaani ambapo Bab alikabiliana na mlolongo wa vifungo, mashitaka, na fedheha kabla ya kuuliwa kwa risasi na kikosi cha watu wanaoua watu waliohukumiwa kifo mwaka 1850.

Mirza Husayn Ali, Bahaullah, alizaliwa mjini Teheran mwaka 1817. Alikuwa ni mtoto mkubwa wa Mirza Abbas wa Nur, Waziri wa Nchi. Alipata elimu ya awali nyumbani na hakupata kwenda shule. Yeye ndiye aliyekuwa mfuasi wa mwanzo na mashuhuri wa Bab na alifungwa jela mwaka 1852 kufuatia jaribio lililoshindwa la wafuasi wa Bab (Babies) kumuua Shah. Bahaulla aliugua sana jela na akapelekwa uhamishoni mjini Baghdad (badala ya kunyongwa) baada ya Waziri wa Urusi kuingilia kati. Viongozi wa Kiislamu wa serikali za Mitaa mjini Baghdad waliyapinga mafundisho na harakati za Bahaulla hadi Mfalme alipomtaka yeye na wafuasi wake kuhamia Constantinople na baadae kuhamia Adianople. Wakati wa safari hii mwaka 1863, Bahaulla akajitangaza kuwa yeye ni nabii, ‘ndiye aliyeahidiwa’ (kama ilivyobashiriwa na Bab) na akakubaliwa na wafuasi wa Bab, sasa wakaitwa wabahai (Bahais). Hata hivyo, kundi moja lililokuwa chini ya Mirza Yahya, mrithi halisi wa Bab, likajikata. Waislamu wakakataa kumkirimu msaliti huyu wa imani ambapo serikali ya Uturuki ililazimika kuwa*****uza wababi na wabahai kutoka Adrianople. Bahaulla na wafuasi wake wakapelekwa kuishi uhamishoni katika mji wa magereza wa Akka nchini Palestina mwaka 1868 wakati ambapo Mirza Yahya na kundi lake walikwenda Cyprus.  Bahaullah akafia huko mwaka 1892 na akarithiwa nas Abdul Baha (Abbas Effendi), mwanawe mkubwa kabisa. Abdul Baha alikufa mwaka 1921 na akarithiwa na mjukuu wake Shoghi Effendi ambaye naye alikufa mwaka 1957 pasina kuwa na mrithi. Wabahai sasa wanaunganishwa na kuongozwa na Taasisi yao ya Haki ulimwenguni.

Mirza Ghulam Ahmad alizaliwa mjini Qadiani (India) mwishoni mwa miaka ya 1830. Alipata elimu yake ya awali nyumbani kwao kutoka kwa walimu wa Kishia na Sunni. Alifanya kazi kama karani wa ngazi ya chini katika ofisi ya Naibu Kamishina (Sialkot) ambako alifeli mtihani wa kupandishwa cheo mara tatu. Katika hali ya kuchanganyikiwa, akaelekea upande wa dini na kuendeleza tabia za kusoma na kujitawisha. Katika kipindi hiki, alikuwa na mikutano kadhaa na Mchungaji Butler,

mmishenari mashuhuri wa Kikristo, kwa ombi la naibu Kamishina. Mara baada ya (1876) Gulam Ahmad alijiuzulu na akarejea mjini Qadiyani kufuatia kifo cha babaake. Katika miongo miwili iliyofuata, alijigeuza na kujifanya mchaMungu, Mujaddid, mtetezi wa imani na akatumia mantiki ya upotoshaji (kama ile ya Bab) ili kujitangaza kuwa yeye ndiye Mahadi aliyeahidiwa, Masihi aliyeahidiwa na mwishowe nabii. Jamii ndogo ya Waislamu wa kawaida, baadhi ya nduguze (mkewe wa kwanza na watoto walikataa kubadili dini), na washirika wake wa karibu walikwenda pamoja naye hadi ndani ya eneo hili ambako aliwatangaza Waislamu walioukataa unabii wake kuwa ni makafiri.  Waislamu thabiti na Maimamu wao wakamlaani na kumtangaza Gulam Ahmad na wafuasi wake kuwa si Waislamu, huu ndio msimamo unaoshikiliwa na takribani nchi zote za Kiislamu. Mirza alikufa mwaka 1908 kwa ugonjwa wa kipindupindu baada ya kuugua magonjwa ya kiharusi, kisukari na yumkini ugonjwa wa wazimu katika miaka ya baadae ya umri wake. Miaka michache baada ya kifo chake, wafuasi wake (Ahmadiya) wakagawanyika makundi mawili, Makadiani na Malahori.  Jamii ya kimajusi (inayonasibishwa na dini za Uzorostani, Uyahudi, Ukristo, Uchaldeani na Usabeani) ilikumbwa na msambaratiko si mara, si mara mbili na kupata kazi ya kujenga upya jamii yake huku ikikumbana na umbambala wa kidini hadi pale Uislamu ulipomkomboa mwanadamu kutoka katika hali hii mbaya ya kuhuzunisha kwa njia ya imani juu ya Mwisho wa Unabii wa Muhammad (saw). Mungu anayesababisha matetemeko ya ardhi na tauni vinapohitajika, nabii anayefanya mambo kama mtabiri, na dhana ya uendelevu wa nguvu ya roho ya Masihi zina chimbuko lao katika Uyahudi wa mwanzo. Kwa mujibu wa Allama Iqbal, dhana hizi ni haramu na ngeni katika Uislamu. Harakati za uzushi nchini Iran zilipata mwanya wa mapengo ya itikadi ya Kishia kwa kuzirejesha upya dhana za kimajusi katika vazi la buruz, hulul, zill na kadhalika. Mbinu hiyo hiyo ikatumika katika bara la Sunni ambako Waislamu, kihistoria, walikuwa wamezikubali dhanna za Kisufi kama vile chilla, kashaf, ilham na kadhalika, kuwa ni sehemu ya Uislamu. Harakati zote mbili za Ubahai na Uahamadiya zilistawi kutokana na ujahili wa Umula na msaada wa siri wa Uingereza katika wakati ambao nguvu ya kisiasa ya Waislamu ulimwenguni ilikuwa ikiporomoka kwa kasi.

Rejea zaidi:

. ‘Roohani Khazain’ by Mirza Ghulam Ahmad Qadiani

. ‘Bahaullah and the New Era’ by J.E. Esslemont

. ‘Qadianies and the Orthodox Muslims’ by Iqbal

. ‘Jhootey Nabi-False Prophets’ by Rafiq Dilawari

. ‘Talbess-e-Ibliis’ by Rafiq Dilawa

Mouvement Anti Ahmadiyya en Islam

Dr Syed Rashid Ali

PO BOX 11560 Dibba, Al Fujairah. U.A.E

E-mail : rasyed@emirates.net.ae/ alhafeez.org/rashd

تاريخ الاضافة: 26-11-2009
طباعة