Anti ahmadiyya Mouvement in Islam
MAANDIKO YAELEZA
Tawasifu ya Mirza Ghulam
MAISHA YA AWALI YA MIRZA QADIANI
" Uzawa wangu ulijiri mwaka 1839 au 1840 A.D. Mimi nilikuwa pacha.
Pacha mwenzangu alikuwa msichana ambaye jina lake lilikuwa jannat
(pepo). Katika ufunuo wangu ‘Ya Adam uskun antaa wa zaujuka’, ambao
ulitajwa katika Brahiin Ahmadiyya ukurasa wa 496, miaka 20 iliyopita, neno
hili ‘jannat’ lilibeba maana hii maalum kwamba msichana aliyezaliwa pacha
na mimi, jina lake lilikuwa jannat ambapo msichana huyu alikufa baada ya
kuishi miezi 7"
Tiryq-ul-Quluub, Roohani Khazain Juz.15 uk. 479 na Mirza Ghaulam Ahmad Qadiani).
"Baba yangu Mirza Ghulam Murtuza alikuwa Mmiliki mashuhuri wa mashamba.
Wakati wa utoto wangu, elimu yangu ilianza kwa namna ambayo nilipokuwa na
miaka 6-7, Mwalimu wa Kiajemi aliajiriwa ambaye alinifundisha Qur’an na vitabu
vichache vya Kiajemi. Jina lake lilikuwa ni Fazl Ilahi. Wakati nilipotimiza umri wa
miaka 10, mwalimu wa Kiarabu (Moulvi) ambaye jina lake lilikuwa ni Fazl Ahmad
akaajiriwa kunifundisha. Nilipokuwa na umri wa miaka 17-18, nilipata fursa ya kupata
elimu fulani kutoka kwa baba yangu. Alinifundisha Sarufi, Mantiki na Tiba (hukmat)
ambapo baadhi ya vitabu vya tiba nilifundishwa na babaangu. Kwa sababu ya afya
yangu, baba yangu, mara kwa mara, alikuwa akinikataza kusoma-soma sana.
"Kuhusiana na vijiji ambavyo serikali ya Mwingereza ilivitaifisha, baba yangu
alifungua kesi katika mahakama ya Mwingereza ili kuvirejesha. Mimi nikateuliwa
kuwakilisha katika kesi hizi. Ingawaje jambo hili halikulingana na kimo changu na
ingawaje sikutaka kupoteza muda wangu mahali hapo pabaya lakini nilililazimika
kufuatilia mashauri hayo ya mashamba. Enzi hizo niliajiriwa na Mwingereza katika
mahakama ya Sialkot kwa miaka michache nikiwa karani kwa ujira wa Rupia 15/-kwa mwezi.
"Baadae nikajiuzulu na, kwa mara nyingine, nikapata kazi katika menejimenti ya
mashamba. Mara nyingi nilikuwa nikiitafakari tafsiri ya Qur’an. Nilipotimiza umri wa
miaka 30-35 babaangu akafariki dunia. Wakati huo mimi nilikuwa mjini Lahore. Baada ya baba yangu kufariki dunia ndipo mfululizo wa mazungumzo na Mungu (Mukalimat-e-llahiah) ulipoanza motomoto."
(Kitab-ul-Bariayh uk 134-136, Summary of commentary (Mukhtasari wa Tafsiri) on margins , by Mirza Ghulam Ahmad Qadiani. Roohani Khazain Juz. 13 uk. 180;
TUZUK-E-AHMADI ulioandikwa katika AKBAR-AL-HAKAM QADIAN Special No, Juz.
37 Na.18519, tarehe 21-28 Mei 1934 AD).
Mirza Atoroka na Fedha za Pensheni: "Bismillah ar- Rahmani ar-Rahiim. Bi Waalida Sahiba (Bi mkubwa yaani mamaaake
Mirza), wakati mmoja, aliniambia kuwa ‘enzi za ujana wake, Masihi Muwuud
alipokwenda kupokea pensheni ya babu yako, binamu yake aliyeitwa Mirza Imamdiin
naye alimfuata. Alipopokea pensheni, basi kwa hila na udanganyifu binamu yake
huyo, badala ya kumpeleka Mirza mjini Qadiani yeye akampeleka nje ya Qadian,
akaenda naye huku na kule na alipotumia fedha zote, Imamdiin akamtelekeza Mirza
na kutorokea mahali fulani. Masihi Muwuud hakurudi nyumbani kutokana na aibu na
kwa kuwa babu yako mara nyingi alimtaka afanye kazi , basi akafanya kazi katika Mahakama ya Naibu Kamishina wa Mji wa Sialkot kwa mshahara mdogo".
(Seeratul Mahdi sehemu ya 1 uk. 41 na Mirza Bashiir Ahmad s/o Mirza Ghulam Ahmad Qadiani)
KUANGUKA KWA FAMILIA "Baba yangu, Mirza Ghulam Murtuza alikuwa akikalia kiti katika jumba la Gavana, na
alikuwa mpenzi wa serikali ya Mwingereza na shujaa katika moyo wake, ambapo
katika uasi wa mwaka 1857 AD, aliisaidia serikali ya Mwingereza, kwa kiasi
kilichozidi uwezo wake, alinunua farasi 50 kwa pesa iliyotoka m*****oni mwake na
kutoa askari wa kujitolea elfu hamsini. Hadhi ya mashamba tuliyomiliki ilikuwa
inashuka siku hadi siku ambapo hadi kufikia zama zetu hadhi ya familia yetu ilikuwa
ya mmiliki ardhi wa daraja la chini". (Tohfa-e-Qaiser, Roohani Khazain juz. 12
uk.270-271).
"Mwingereza alitaifisha ardhi ya familia yetu na akaweka pensheni ya heshima ya
Rupia 700/- tu kwa mwaka kwa fedha taslimu ambayo ilipunguzwa hadi Rupia 180/-
alipokufa Babu yangu na ikasita kabisa baada ya kifo cha babaangu mkubwa."
(Seerat-ul-Mahdi, Sehemu ya 1 uk.41 na Mirza Bashiir Ahmad s/o Mirza Ghulam Ahmad Qadiani)
MARADHI YA YULE ALIYEAHIDIWA "Magego yake (Mirza Ghulam Qadian) yalikuwa na uozo ambao ulikuwa ukimletea
maumivu mara kwa mara ambapo jino moja lilichongoka na kusababisha kidonda kwenye ulimi wake, ikabidi lichongwe."
(Siirat-ul-Mahdi sehemu ya ii uk. 135 Na Mirza Bashiir Ahmad s/o Mirza Ghulam Ahmad Qadiani).
" Aliwahi kudondoka kutoka dirishani na kuumia mkono ambao ulilemaa hadi mwisho."
(Siiratul-ul-Mahdi sehemu ya ii uk. 198)
UKHANITHI « Kikongwe huyu ana maradhi ya ulemavu wa ubongo. Kwa muda mrefu baada ya kuoa, nilikuwa nikijiona khanithi ».
(Barua ya Mirza Ghulam Ahmad tarehe: 22/2/1887 katika Makhtoobate Ahmadiyya Juz. 5, uk. 14 iliyonakiliwa kutoka Navishta-e-Ghaib by Khalid Wazirabadi)
"Wakati wa ndoa, moyo na ubongo wangu vilizorota sana na nikawa nasumbuliwa na kizunguzungu, haya yamekuwa nami kwa muda mrefu; kwa sababu ya haya, nikapata uchungu (huzuni) ya unyong’onyevu wa moyo na ukosefu wa nguvu za kiume."
(Tiryaq-ul-Quluub Roohani Khazain Juz. 15 uk 203 By Mirza Ghulam Ahmad Qadian).
Akimwandikia Hakiim Nuuruddin, Mirza kasema hivi:
"Napata nafuu kubwa kwa dawa zako. Magonjwa machache kama uchovu na asidi tumboni yametibika kwa dawa hizo. Nilikuwa na tatizo moja kubwa sana kwamba urijali wangu ulikuwa unapungua wakati nilipokuwa nikilala chini kwa ajili ya ngono. Ukosefu wa nguvu za kiume ndio uliosababisha hilo. Hivyo, kwa dawa zako nguvu zangu za kiume zimerudi."
(MAKHTOOBAT-E-AHMADIYYA Juz 5. Na. 2 Mkusanyo wa Barua za Mirza Ghulam Ahmad Qadiani).
"Wahayi ulishushwa kwangu kuhusiana na ndoa; wakati huo moyo na ubongo na mwili wangu vilidhoofu sana. Mbali ya ugonjwa wa kisukari na kizunguzungu kichwani na huzuni ya (unyong’onyevu) wa moyo, pia nilikuwa naugua kifua kikuu."
(Nuzuul-e-Masiih, Roohani Khazain juz. 18. uk. 587 tanbihi ya Mirza Ghulam Ahmad Qadiani).
" Yeye (Mirza Ghulam Ahmad Qadiani) alikuwa akifunga swaumu mara chache mwezi wa Ramadhani ambapo fidia ilitolewa; na kwa sababu ya ugonjwa, alifungua swaumu moja muda wa Magharibi. Alikuwa akipata magonjwa mara kwa mara na afya yake, kwa ujumla, ilizorota."
(Siirat-ul-Mahdi sehemu ya i uk. 51 iliyoandikwa na Mirza Ghulam Ahmad Qadiani).
"Hazrat Sahib alikuwa mgonjwa sugu wa unyogovu. Ugonjwa huu ulikuwa wa kurithi.
(Mirza Sahib hakuweza kuubeba mzigo wa Utume!!-Mwandishi). Mirza alikuwa na
mjomba wake ambaye jina lake lilikuwa ni Mirza Jamiat Baig. Alikuwa na mtoto
mmoja wa kiume na binti mmoja na wote wawili walikuwa na maradhi ya akili. Jina la
mtoto wa kiume lilikuwa ni Mirza Sher Ali. Wa kike alikuwa Hurmat Bibi. Binti huyu
akaolewa na Bwana Sahab" (Mirza na mkewe Hurmat Bibi-wote wawili machizi! Hiki lazima kiwe ni kiroja kikubwa! Na watoto waliotokana nao je?- Mtu anaweza kupata picha-Mwandishi)
(Siirat-ul-Mahdi sehemu 1 uk. 51).
UGONJWA WA UNYOGOVU KATIKA VITABU VYA KALE VYA TIBA Unyogovu (depression), yumkini, umekuwa sehemu ya hali ya mwanadamu kwa
kipindi chote ambacho mwanadamu amekaa duniani. Hata usomaji mdogo tu wa
maandiko ya awali wabainisha maelezo juu ya unyogovu. Waandishi wa zamani
waliyatambua baadhi ya matatizo hayo ambayo sisi, baada ya miaka 2,000 hadi
4,000 ndiyo tunayatibu. Maandiko mengi ya Wagiriki yaliielezea dhanna ya unyogovu
ulioshushwa na Mungu.
Lakini miaka 2,300 iliyopita, Hippocrates alitambua kuwa matatizo ya kiakili yanatokana na sababu za kimaumbile badala ya mabadiliko ya nguvu za Kiungu.
Istilahi yake ya magonjwa ya akili bado inatumika hivi leo; epipepsy (ugonjwa wa
imani); mania (machepele), Melancholia (unyong’onyevu unaotokana na nyongo
nyeusi) na paranoia (kipaipai). Hippocrates pia kamuelezea mwanamke mmoja
aliyerukwa akili kwa unyong’onyevu ambaye alipata tatizo la kukosa usingizi, kukataa
chakula, kiu na kichefuchefu. Orodha hii ya kale ya dalili za unyong’onyevu inatoa
tahadhari kabla ya maelezo ya sasa ya ugonjwa wa unyogovu (depression).
Enzi za Warumi, daktari mmoja wa magonjwa ya binadamu, Galen, aliandika kuhusu
unyogovu. Katika kuielezea hali ya unyong’onyevu, Galen alisema kuwa wagonjwa
kadha wa kadha huonesha hofu, unyong’onyevu, kutoridhika na maisha, na kuchukia
watu wote Yeye alidai kuwa misukumo ya njozi za kufanya mambo yasiyowezekana
ilionekana katika ubongo ambao, moja kwa moja, uliathirika kwa unyong’onyevu.
Katika maelezo haya ya ensaiklopedia, Galen anajumuisha magonjwa ya dyshmia
(kisirani), crasis (khulka), na (uchepe). Kitabu cha Robert Burton, "Anatomy of
Melancholia", kilichochapishwa mwaka 1630, kilieleza kwa mukhtasari kile ambacho,
kwa wakati huo, kilijulikana kama Unyogovu na kikaainisha unyong’onyevu kama ni
"maradhi ya kichwa au akili" mara nyingi, yakinasibishwa na maumivu na huzuni.
Burton akaifagilia njia elimu ya baadae ya sayansi juu ya unyogovu na akaorodhesha
sababu za unyogovu ikiwa ni pamoja na zile za kisaikolojia kama vile aibu, soni, ghadhabu, kujipenda na kujitesa.
Mchango mwingine muhimu katika maelezo ya unyogovu ulitolewa na Freud katika
kitabu chake, Mourning and Melancholia kilichochapwa mwaka 1917. Freud aliandika
kuwa unyong’onyevu ulibainisha majuto yanayoanzia katika uchaguzi wa kitu hadi
utaratibu duni wa kujinasibisha na vitu. Maelezo yake juu ya "unyogovu wa njozi"
yanashadidia dukuduku la moyoni linalochukua nafasi ya hasira ambazo zingepaswa
kuelezwa bayana. Yeye aliamini kuwa watu wanaosumbuliwa na unyogovu hujitesa
wenyewe bila huruma huku wakiyahusisha mateso hayo na mtu mwingine kama vile
kuyahusisha na kiungo cha uzazi ambacho labda wamekipoteza. Mtu sasa anaweza
kupata picha ya kile ambacho kingemtokea Mirza kama Freud angepata fursa ya kumchunguza Mirza!
Unyogovu umeelezewa kwa maelfu ya miaka, kwanza na washairi na wanafalsafa na
hivi karibuni tu ndio umeelezewa na madaktari wa magonjwa ya binadamu. Leo hii
tumeingia katika zama ambazo maelezo kuhusu magonjwa yanachangiwa na utafiti
unaofanywa na taasisi za tiba na wanasayansi.
« Kulingana na mtazamo wa Hikmat na Ugiriki, ugonjwa huu hutokea kwa sababu ya
mkusanyiko wa nyongo nyeusi tumboni. Katika kiungo chochote inapokusanyika nyongo hii, mvuke mweusi hutokea na kupanda hadi ubongoni. Dalili zake ni:
kilungulia, kihoro cha unene hasa kwa wanawake kinachowafanya waache kula na
kuhatarisha maisha yao kwa sababu ya kudhoofu kwa tumbo, kuvurugika kwa
mfumo wa usagaji, uvimbe wa tumbo, mwendo wa hovyo, kuhisi moshi kama vile
mvuke unapanda ndani." (Je wahai na ufunuo wa Mirza ulitokana na mivuke hii?-Mwandishi). (Guide to causes & symptoms of Melancholia (Muongozo wa sababu na dalili za Unyogovu) by Allama Burhanuddin Nafees).
"Ilidhaniwa kuwa dalili za ugonjwa huu wa (unyong’onyevu) husababishwa na
udhaifu katika nguvu za kuhamasisha ngono ambazo ni ini na tumbo. Lakini utafiti
wa hivi karibuni umeonyesha kuwa huo ni ugonjwa wa akili kama vile umanyeto kwa
wanawake. Kasoro katika viungo vya ndani hupelekea katika udhaifu wa akili
unaosababisha unyong’onyevu kwa wanaume. Dalili zake: Mgonjwa mara zote huwa
mnyanyapavu wa vitu, huwa mwenye kuona wasiwasi, mara zote, akilikweza kwa
maelezo kila jambo.......huku akiwa hana hamu ya kula na uyeyushaji wa chakula
mwilini ukiwa katika hali mbaya”. (Makhzan-e-Hikmat, kilichoandikwa na Hakiim Dkt.
Gulam Jiilani).
"Usagaji hafifu wa chakula mwilini, kilungulia, sailorea, borbarigami, uvimbe tumboni,
kichomi, kuwa na uchu mbaya, kuhisi mvuke wa moshi ukipanda kichwani, dalili za
kupungua kwa unafuu wa uyeyushaji wa chakula mwilini, dalili za kuongezeka kwa
tatizo la uyeyushaji chakula mwilini, wakati mwingine, hutokea mishituko katika
viungo vya juu vya mwili, mikono na miguu na wakati mwingine mwili mzima huwa
baridi, kulingana na hatua iliyofikia ugonjwa, mwili hudhoofu, mara kwa mara mgonjwa huona miale ya mwanga mbele ya macho, mboni za macho huwa nzito, hujihisi joto na kuchomwa-chomwa kichwani na ubongoni, maumivu ya kichwa na kupaliwa kwa ghafla, zote hizi ni dalili za unyogovu."
(Akseer-e-azam, juz; 1, uk. 189 iliyoandikwa na Hakiim Mohammad Azam Khan)
Umesoma maudhui ya hapo juu kuhusu ugonjwa huu. Namuomba kila mtu, kwa
mtazamo sahihi, ayachukulie madai ya ufunuo, wahai na maongezi na Mungu
yaliyotolewa na Masihi huyu kuwa ni porojo tupu za mtu punguani na jitenge mbali na
mgonjwa huyu wa unyogng’onyevu anayeitwa mtume ili uweze kuwa Muislamu wa
kweli na kuepukana na laana ya kufuru na hivyo kuwa muumini na mfuasi mwaminifu
wa Mtume Muhammad (saw). Mtume (saw) kasema:
"Katika Umma wangu, kutakuwa na wazushi wapatao 30 na kila mmoja wao atasema
kuwa yeye ni nabii wa Mungu. Sasa ni juu yenu kubaini huyu ni mtu wa ngapi."
Sasa hebu tuone wasomi wengine wanasemaje juu ya Unyong’onyevu.
AVICENIA (ABU ALI SENA) Anasema :
"Unyong’onyevu ni ule ugonjwa ambao mawazo na fikira zisizokuwa za kawaida huzuka. Sababu yake ni kufifia kwa uchangamfu kiasi kwamba akili huruka na mgonjwa hufazaika sana kwa kufifia huko. Au kwa namna nyingine ugonjwa huu husababishwa na joto la kupita kiasi la ini. Ugonjwa huu unaitwa hypochonriasis.
Wakati uchafu wa chakula na gesi unapochanganyika katika matumbo, husababisha
kitu cheusi na pale mvuke kutoka katika kitu hicho unapopanda ubongoni, hii huitwa
unyong’onyevu wa gesi (Gaseous melancholia)"
(Canon in Medicine, Fun-e-Awwal from book 3, ABU Ali Sena (Avecina).
Tiba: Ni jambo la lazima kwa mgonjwa wa unyong’onyevu kujishughulisha na kazi ya
kuufanya moyo wake uridhike na azunguukwe na watu wa kumpa heshima na
kumliwaza. Kiasi kidogo cha mvinyo iliyochanganywa na maji kitolewe kwake kwa
wastani."
(Canon in Medicine by Avicena)
Tanbihi : Mirza Ghulam Ahmadi Qadiani alikuwa akitumia mvinyo ya toniki na afyuni kwa sababu hiyo.
"Unyong’onyevu ni mabadiliko ya fikra kutoka katika hali ya kawaida kutokana na hofu na maradhi. Kwa baadhi ya wagonjwa ugonjwa huendelea kiasi kwamba mgonjwa hudhani kuwa anaweza kuzungumzia mambo ya ghaibu na mara nyingi huzungumzia nini kitakachotokea siku za usoni. Baadae ugonjwa huu huendelea katika kiwango ambacho mgonjwa anajiona yeye ni malaika."
(Guide to the Aetiology&Manifestations of desease of Melancholia by Allama Burhanuddin Nafees).
Maono ya ajabu ajabu ya mgonjwa, mara nyingi, hunasiabiana na mambo aliyokuwa
akiyafanya wakati wa uzima wake. Mathalani, kama mgonjwa alikuwa mtu wa dini,
hudai utume na uwezo wa kufanya miujiza, huzungumzia uungu na kuwahubiria watu
mambo hayo." (Askeer-e-Azam Juz 1 uk 188, by Muhammad Aza Khan).
"Kwa mzushi wa ufunuo, iwapo jambo hili linathibitishwa kuwa anasumbuliwa na
Umanyeto, Unyogovu au Kifafa, basi huna haja ya kuhitaji ushahidi mwingine wa
kuukataa utume wake, kwani hili ni pigo ambalo kwalo jengo zima la ukweli
husukumwa mbali na msingi wake". (Na Dkt. Shahanawaz Qadiani in Magazine
Review of Religions, Qadiani Tarehe, Agosti 1926 A.D.).
MIRZA QADIANI NA POMBE + ULEVI WA DAWA ZA KULEVYA " Afyuni (opium), mara nyingi, hutumika katika Dawa za tiba ambazo Masihi (Mirza
Ghulam Ahmad Qadiani) alikuwa akisema kuwa mbele ya macho ya madaktari,
afyuni ni nusu ya tiba. Hivyo, matumizi ya afyuni kwa tiba na si kwa ulevi hayapingwi
kwa namna yoyote ile. Kila mmoja wetu. kwa kujua au kwa kutojua, ametumia afyuni
kwa kiwango Fulani”.
“Hazrat Masiih Muwuud (Masih Mirza Ghulam Ahmad Qadian aliyeahidiwa) alifanya
tiba ya Tiryaq-e-llahi kwa maelekezo kutoka kwa Mungu na kichanganyio chake kikubwa kilikuwa ni afyuni; na dawa hii, baada ya kuongezewa afyuni, akapewa Hazrat Khalifa (Khalifa wa kwanza Hakiim Nuuruddin), alipewa na (Mirza Qadian)
kwa zaidi ya miezi sita na yeye mwenyewe alikuwa akiitumia wakati wa matatizo ya
maradhi".
(Article by Mian Mahmuud Ahmad Khalifa Qadian in Akber Al Fazal, Qadian, Juz 17 Na 6, Julai 19, 1929).
Pombe ya Toniki “Ndugu yangu Mohammad Hussein Sahib
Mungu akulinde, Assalam-O-Alaikum
Yar Muhammad Mkuu sasa anatumwa. Vitu vya kununuliwa, nunua wewe
mwenyewe na nunua chupa moja ya Mvinyo ya Toniki Dukani kwa Plommer lakini
mimi nahitaji Mvinyo ya Toniki zingatia hili. Nyingine ni O.K” (Imesainiwa: Mirza Ghulam Ahmad Qadiani)
(Barua za Imam kwa Katibu Mukhtasi. Mkusanyiko wa Barua za Mirza Ghulam
Ahmad Qadiani kwa Hakiim Mohammad Hussein Qadiani, mmiliki wa zahanati Rafiqus-
Sehat Lahore)
"Undani halisi wa Mvinyo ya Toniki ulichunguzwa kutoka dukani kwa Plommer mjini
Lahore kupitia kwa Dkt. Aziz Ahmad aliyeandika jibu hili :
‘Kwa maagizo, nilichunguza Dukani kwa Plommer na jibu ni hili lifuatalo:
"Mvinyo ya Toniki ni aina ya mvinyo kali na ya kulevya ambayo huagizwa kutoka
Uingereza (U.K. Wilayat) katika chupa zilizozibwa. Bei yake ni Rupia 5 Annas 8 (21/9/1933)."
(Sauda-e-Mirza uk. 39 By Hakiim Mohammad Ali, Mkuu wa Chuo, Tibbiya College Amratsar)
Hebu ona jinsi inavyodhihirika kuwa madai ya Mirza kwamba yeye ni Masihi
aliyeahidiwa, Mahdi na Nabii yalikuwa ni dalili za maradhi na hayakutokana na
ufunuo wala mazungumzo na Mungu. Tatizo hili likazidishwa na matumizi ya Afyuni
na Mvinyo ya Toniki. Namuomba MwenyeziMungu awape mwongozo na ufahamu
Makadiani ili wafuate njia sahihi. Vinginevyo wafuasi wa mgonjwa wa unyong’onyevu,
nao pia watakuwa wanyong’onyevu.
Mouvement Anti Ahmadiyya en Islam
Dr Syed Rashid Ali
PO BOX 11560 Dibba, Al Fujairah. U.A.E
E-mail : rasyed@emirates.net.ae/ alhafeez.org/rashd