BismillahRahmanir Rahiim
Anti Ahmadiyya Movement in Islam
Albania brother leaves Ahamadiyya Belgium
Kijana kialbania aeleza jinsi alivyoachana na ukadiani nchini ubelgiji
muqadima
kwa jina naitwa Rinol kwa asili mimi ni mualbania ninatokea Macedonia .Hivi sasa ninasoma nchini ubelgjji kama walivyonaswa watu wengine wengi ;mimi pia niliangukia kwenye mtego wa dajjali wa
ukadiani.
Ukadiani kama unavyojulikana ni kikundi cha watu wachache wanaojinasibisha na waislamu hasahasa wale wanaoishi ulaya mashariki ndio walio hatarini kuathirika na imani ya ukadiani. Inafahamika kwa kila mtu kuwa kiutawala waislamu wa ulaya mashariki wameishi kwa sheria ya kikomunisti ya kuishi bila dini. Kwa hili nathubutu kusema kuwa sikuwa tayari kabisa kuipinga imani ya ukadiani. Mwaka 2000; kijana mmoja wa kikadiani akanipa habari za dhehebu lake ambalo kwa kweli mwanafunzi huyu kikadiani akaniambia kuwa katika nyumba mnamofanyikia shughuli za makadiani wanavyo vitabu vilivyoandikwa katika lugha ya kialbania. Mimi nikavutiwa na jambo hilo kwani kwa muda mrefu nilikuwa sijasoma vitabu vya aina yoyote vilivyoandikwa katika lugha ya kialibania. Kumbe wote huo ulikuwa ni ujanja wa kunizuga kwani nia hasa ilikuwani kunipeleka huko nikazungumza na madokta wa kikadiani waliobobea katika kazi yakuvuruga bongo za vijana wa kiislam wa ulaya mashariki. Lakini mimi nasema wazi kuwa makadiani hawajafanikiwa kabisa kueneza imani yao miongoni mwa waislamu wanaoishi ulaya mashariki. Wengi kati ya wale walioingia katika ukadiani sasa wametoka. Mimi mwenyewe nilikaa katika ukadiani miezi mitano tu. Sitaeleza namna nilivyoangukia mtego wa makadiani bali nitaelezea jinsi nilivyojinasua katika mtego huo. Ni mwishoni mwishoni mwa miezi hiyo mitano ndipo mimi nilipoanza kutanabahi kwamba nilikuwa katika mtego fulani. Kadri nilivyozidi kusoma mambo mapya ndivyo nilivyozidi kuujua ukadiani na makadiani kwa ujumla. Ikazidi kunidhihirikia kuwa ni kitu kisicho sahihi. &n bsp; Kwanza kabisa mimi nilikuwa sijuwi kuwa baada ya kifo cha mwanzilishi wa ukadiani. Makadiani waligawanyika makundi mawili. Pili makadiani walikuwa wakiwazungumzia vizuri mayahudi lakini wakati huo huo wao haohao walikuwa wakitoa maneno makali na ya kudhalilisha dhidi ya waislam kuwa ni makafiri. Isitoshe kadiani haruhusiwi kuswali nyuma ya Imamu
muislamu. &n bsp; Kitu ambacho mimi sikukielewa ni kwanini mayahudi wawe wateule wakati ndio hao waliojaribu kumuua nabii Issa [as]/ zaidi ya hivyo wanaweza kuwa wateule ikiwa wao hao ndio waliompigia vita mtume wetu Muhammad [saw] na mpka sasa wanafanya mbinu kubwa kupiga vita uislamu na juu ya hivyo qur- ani tukufu inaeleza waziwazi kuwa mayahudi ni maadui wa uislamu. Kutokana na maandiko [fasihi andishi] yao nikagundua kumbe makadiani walikuwa na mahusiano mazuri sana na waingereza katika kitabu chake kiitwacho. Invitation ton Ahmadiyyat; mtoto wa Mirza Ghulam anaelezea ukweli kuwa yeye alikuwa akiiombea dua dola ya uingereza ishinde vita vya kwanza vya dunia. Je India haikufanywa koloni la waingereza/ Nadhani lingekuwa jambo la maana kama angeomba uingereza ishindwe vita Kwa hiyo hii ikanibainishia kuwa lazima tu kuwe na mahusiano ya aina fulani kati ya makadiani na wakoloni wa kiingereza. Baadae tena nikaona kitabu kiitwachoAhmadiyya Movement: British Jewish Connections kitabu hicho kimeandikwa na Bashir Ahmad ambae ni muislamu kitabu hicho kilinisaidia sana kuelewa kuwa ukadiyyani ni upotovu mkubwa kabisa kitabu hicho kilinisaidia kutoka katika maisha ya udanganyifu[ukadiyyani] khaswa khaswa nilifurahi kupata ushahidi kuwa makadiyyani wana mahusiano madhubuti na mayahudi ni pia ni vibaraka halisi wa waingereza ndani ya uislamu Allah anasema katika Qura an
Enyi mlioamini! msiwafanye wayahudi na wakristo kuwa marafiki zenu[wa kuwapa siri zenu]wao kwa wao ni marafiki na miongoni mwenu atakayefanya urafiki huo nao basi huyo atakuwa pamoja nao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu[5:51]
Ndoto Miezi 6 kabla sijawa kadiani niliota ndoto ambayo ilikuwa ya kueleweka kabisa katika ndoto hii nilimuona Mtume Mtukufu Muhammad SAWS] amesimama mbele yangu ijapokuwa hakusema yeye ni nani mimi nikajua kabisa alikuwa yeye.
Nilifurahi sana kuota ndoto hiyo njema hapo kabla sikupata kuota ndoto ya aina hiyo katika ndoto hiyo niliona wingu la buluu kama lile la hasubuhi na mwangaza wa jua Mtume wetu Muhammad alivaa mavazi meupe yenye mistari stari michache ya kijivu alikuwa na nywele nyeusi na sura yenye mvuto Muhammad [SAW] akazungumza kwa lugha yangu ya asili [kialbania]akinambia ‘wewe utapata ‘garth[sijapata kulisikia neno hilo] hapo hapo nikaamka nikamuona mjomba akienda zake kazini mapema mno hasubuhi nikamuuliza mjomba hivi neno hili lina maana gani akaniambia ni uzio unaozunguuka nyumba [fensi] mara nyingi kwa ajili ya kondoo au wanyama wengine naye kaka yangu mkubwa nilipomuuliza alinijibu hivyo hivyo ila yeye akaongeza tu anaweza kuwa ni uzio unaotumika kwa ajili ya usalama
Nilipokuwa kadiani ndoto hii haikunijia kichwani nikamsimulia ndoto hii kiongozi wa kadiyyani mhadhiri huyo akaniambia eti niliyemuona ndotoni ni Mirza Ghulam au mmoja wa viongozi [makhalifa]wanne wa dini ya kadiyyani mimi nikawajibu kwa kuwaambia kinagaubaga kuwa yule si mwingihne bali alikuwa mmbora wa viumbe Mtume Muhammad[SAW] ndiye niliyemuona ndotoni.
Nilipoota ndoto hii tayari nilikwishayajua mambo fulani kuhusiana na harakati za ukadiyyani kupitia kwa mwanafunzi mwenzangu huyu mwanafunzi alinitia mashaka juu ya ujaji wa ya ujio wa Imam Mahd mimi nikampa jibu hili baada ya hapo yeye akaniandkia kuniambia kuwa ‘si mimi asilani niliyekuotesha ndoto hizo hizo bali ni Allah kwa hiyo kama unataka kulaumu basi mlaumu Allah aliyekuleta katika njia hii ya ukadiyyani” mimi nikaendelea kuwajibu kuwa kwa hakika ile ndoto niliyoota alikuwa si mwingine bali ni Mustafa Muhamma[SAW] viongozi wa jumuiyya ya Ahmadiyya wakaendelea kunieleza kwa kuniambia ‘hivi wewe una hakika kweli sio Mirza ghulam aliyekutokea ndotoni au sio mmoja wa makhalifa wake?” nikaendelea kuwajibu kuwa je ndoto hiyo hawezi kuoteshwa mtu atakayejitoa katika njia ya Ahmadiyya je mwaweza kusema kuwa ndoto hiyo ndio wanaoteshwa watu wenye kufuata itikadi ya kadiyyani peke yake labda ninyi makadiyyani mwaweza kuniambia mbona mimi nimejitoa katika njia yangu ya uislamu na kuingia katika jumuiyya ya Ahmadiyya ni kweli nakubali mimi nilitoka katika njia ya uislamu lakini ikaja kunibainikia dhahiri kuwa shahiri kwamba ukadiyani ni upotevu wa wazi kabisa na ni ukafiri pasina shaka
Kisa cha mwisho Mirza Ghulam wa kadiyyani aliandika kitabu kiitwacho ‘The philosophy of teaching of islam”[falsafa ya mafundisho ya uislamu] kiongozi wa shura akapendekeza nisome kitabu hiki baada ya mimi kuwaomba wanipatie vitabu vilivyoandikwa na mwasisi wa ukadiyyani tokea utotoni mwangu hii ilikuwa ni mara ya kwanza kusoma kusoma kitabu kilichoandikwa na mwanzilishi wa dini ya ukadiyyani.
Kwa rehema za Allah kitabu hiki kidogo kikanipa maelezo ya kutosha kumbaini mtu muongo na muhalifu wa misingi ya uislamu katika tafsiri ya kiingereza ya kitabu hiki jambo ambalo mimi limenishangaza ni tafsiri ya sura 102 ya qur an [surat takathur ambayo ina aya 8] Mirza ameifasiri vibaya mno tena ovyo kabisa.
Amefanya hila kubwa ili kuipa nguvu tafsiri anayoitaka yeye mwishoni ameongeza jambo ambalo halikuelezwa kabisa katika aya zote na nalo ni “ninyi mtaijua jahanam kutokana na hisia zenu” [Taz.Ahmad Mirza Ghulam;The philosophy of teaching of islam London[1992]uk.75]kwa kweli huu ni uhalifu mbaya sana na mtu mwovu tu ndiye anayeweza kuthubutu kufanya hivi kwa hiyo Mirza Ghulam Ahmad ni DAJJAL[mrongo mkubwa]kwa sababu hii ndio maana mimi nimejitoa kwenye mtego wa makadiyyani.
Maelezo yangu kuhusu hali ya ukadiyyani nchini Ubelgiji
Kiongozi wa harakati za ukadiyyani pamoja na kiongozi wa shura wamekataa katakata kunipa maelezo kuhusu idadi ya makadiyyani nchini ubelgiji ninaposema kukataa sina maana kuwa wamesema hatuwezi kukupa idadi hiyo bali wanapiga chenga kujibu wazi kuwa ukadiyyani hauna nafasi ubelgiji. Kwa utafiti wangu makdiyani kwa hapa wako200 tu[wakiwemo na watoto wao]wengi wao wanatokea Pakistan wasio wapakistan walioingiakatika ukadiyyani ni 10 tu katika kipindi cha miezi mitano ya kuwemo kwangu katika ukadiyyani nilishuhudia watu wawili wakijitoa katika jumuiyya hii ya upotovu watu hao sikuwaona tena wakija kituoni kwa miezi chungu mzima mimi nilimuuliza kiongozi wa shura je vijana hao wawili wako wapi akawa hana jibu kabisa la kunipa.
Huu muhtasari tu sikueleza mengi sana yaliyonipelekea kuuona ukweli na hatimaye kuuacha ukadiyyani na kurejea katika uislamu mapungufu yote niliyoyagundua kunahitaji ufafanuzi wa kina kwa hiyo nitawaleza zaidi mengi yaliyomo katika ukadiyyani InshaAllah nitawaelezeni siku nyingine